Surah Hud aya 45 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ﴾
[ هود: 45]
Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And Noah called to his Lord and said, "My Lord, indeed my son is of my family; and indeed, Your promise is true; and You are the most just of judges!"
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote.
Huruma ilimshika Nuhu moyoni mwake kwa ajili ya mwanawe. Akamwomba Mola Mlezi wake kwa unyenyekevu na kuona huruma, akasema: Ewe Muumba wangu, uliye nianzisha nami sijawa chochote! Hakika huyu mwanangu ni kipande cha nafsi yangu, naye ni katika ahali zangu. Na Wewe umeahidi kuwa utawaokoa ahali zangu, na ahadi yako ni ya kweli, madhubuti, lazima iwe. Na hapana muadilifu kama Wewe! Kwani Wewe ndiye Mjuzi kushinda wote, na Wewe ni mwingi wa hikima kuliko wote wenye kuhukumu!
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!
- (Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
- Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.
- Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika
- Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
- Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na
- Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili
- Lakini walio mcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizo jengwa juu ya ghorofa; chini yake
- Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
- Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



