Surah Hajj aya 47 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَلَن يُخْلِفَ اللَّهُ وَعْدَهُ ۚ وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ﴾
[ الحج: 47]
Na wanakuhimiza ulete adhabu, lakini Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake kabisa. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi.
Surah Al-Hajj in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And they urge you to hasten the punishment. But Allah will never fail in His promise. And indeed, a day with your Lord is like a thousand years of those which you count.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wanakuhimiza ulete adhabu, lakini Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake kabisa. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi.
Na makafiri wa Makka wameshikwa na udanganyifu, na hawana wanalo litambua juu ya kuwepo dalili zote hizi. Kwa hivyo ndio wanakuhimiza, wewe Nabii, uwaletee adhabu ulio waahidi. Wanasema hayo kwa upinzani na kejeli. Na hayo hapana shaka yoyote yatawapata, lakini kwa wakati alio uweka Mwenyezi Mungu, ama duniani au Akhera. Naye hendi kinyume na ahadi yake, hata ikipita miaka. Kwani siku moja kwake ni kama miaka elfu mnayo ikadiria na kuihisabu. -Na wanakuhimiza ulete adhabu, lakini Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake kabisa. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi.- Qurani kwa Aya hii tukufu imeutangulia msafara wa wana sayansi kwa kueleza kuwa zama ni kipimo cha mnasaba, na kwamba fikra ya kuwa zama kwa ulimwengu ni moja kama watu wa zamani walivyo kuwa wakifikiri ni makosa.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
- Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na
- Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
- Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
- Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa
- Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala
- Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
- Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.
- Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara,
- Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi hao watapata adhabu
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hajj with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hajj mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hajj Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



