Surah Tawbah aya 25 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴾
[ التوبة: 25]
Hakika Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni kitu. Na ardhi ikawa dhiki kwenu juu ya upana wake. Kisha mkageuka mkarudi nyuma.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah has already given you victory in many regions and [even] on the day of Hunayn, when your great number pleased you, but it did not avail you at all, and the earth was confining for you with its vastness; then you turned back, fleeing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni kitu. Na ardhi ikawa dhiki kwenu juu ya upana wake. Kisha mkageuka mkarudi nyuma.
Hakika Mwenyezi Mungu amekunusuruni na maadui zenu mara nyingi katika vita kwa nguvu ya Imani yenu. Na mlipo ghurika na wingi wenu katika vita vya Hunayni, kwanza Mwenyezi Mungu alikuachieni wenyewe. Wingi wenu usikufaeni kitu. Adui akakushindeni, na kwa shida ya kufazaika mkaiona ardhi kuwa ni nyembamba. Msiweze kupata njia ya kupigana wala kuokoka kwa murwa. Wengi wenu wakawa hawana njia ya kuepuka ila kukimbia. Mkakimbia kwa kushindwa, na mkamuacha Mtume na Waumini wachache tu. Vita vya Hunayni walipigana Waislamu na kabila mbili za Thaqiif na Hawaazin. Jeshi la Waislamu lilifika kiasi ya watu elfu kumi na mbili, na makafiri walikuwa elfu nne. Nao walipigana kwa ukali kwa kuwa ilikuwa wakishindwa wao basi ibada ya masanamu itatoweka kabisa kwa Waarabu, kwani Makka ilikuwa ndio kwanza kwisha tekwa. Majeshi mawili yakapambana, Waumini kwa wingi wao, nao uliwapandisha kichwa; na wale makafiri na uchache wao wakali. Kwanza makafiri wakashinda kwa kuwa Waislamu walighurika kwa wingi wao wakajiona. Lakini mwishoe vita vikaishia kwa kushinda Waumini. Funzo la hapa ni kuwa wingi sio unao pelekea ushindi, lakini nguvu za kimoyo na imani.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu Yunus?
- Na kivuli kilicho tanda,
- Wala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi,
- Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
- Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
- Anaingiza usiku katika mchana, na anaingiza mchana katika usiku. Na Yeye ni Mwenye kuyajua yaliomo
- MWENYEZI MUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye
- Na tungeli waongoa Njia iliyo nyooka.
- Tulifanya agano na Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipo wajia Mtume kwa wasio
- Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers