Surah Anfal aya 66 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الْآنَ خَفَّفَ اللَّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ﴾
[ الأنفال: 66]
Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Now, Allah has lightened [the hardship] for you, and He knows that among you is weakness. So if there are from you one hundred [who are] steadfast, they will overcome two hundred. And if there are among you a thousand, they will overcome two thousand by permission of Allah. And Allah is with the steadfast.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
Ilivyo kuwa ni waajibu wenu enyi Waumini, kusubiri mnapo kutana na maadui zenu katika hali ya kuwa mna nguvu, ijapo kuwa wamekuzidini mara kumi, sasa Mwenyezi Mungu amekuruhusini katika hali isiyo kuwa ya nguvu, kuwa mvumilie ikiwa adui kakuzidini mara mbili basi. Hayo ni kwa kukujua kwake kuwa hamna nguvu nyingi, kwa hivyo mmefanyiwa wepesi na mmesahilishiwa, baada ya kuwa heba ya Uislamu imeingia katika nafsi za makafiri. Kwa hivyo mkiwa nyinyi ni wapiganaji mia wenye kusubiri mnaweza kuwashinda makafiri mia mbili. Na mkiwa elfu moja mtawashinda elfu mbili, kwa Mwenyezi Mungu kupenda na kusaidia. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri kwa nusura yake na kuunga mkono kwake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na walisema walio kufuru: Hatutaiamini Qur'ani hii, wala yaliyo kuwa kabla yake. Na ungeli waona
- Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
- Lakini tukiwaondolea adhabu mpaka muda fulani wao waufikie, mara wakivunja ahadi yao.
- Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida
- Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
- Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa
- Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu wema.
- Kimbilieni msamaha wa Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni kama upana wa
- Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.
- Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers