Surah Nahl aya 66 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ﴾
[ النحل: 66]
Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi mazuri kwa wanywao.
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And indeed, for you in grazing livestock is a lesson. We give you drink from what is in their bellies - between excretion and blood - pure milk, palatable to drinkers.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi mazuri kwa wanywao.
Na enyi watu! Hakika katika nyama hoa, yaani mifugo, ngamia, ngombe, na kondoo na mbuzi, mna mawaidha yanayo faa kuzingatiwa na kufuatwa uwongofu wake wa kumtoa mtu ujingani akaingia kumjua Mwenye kuumba, Aliye anzisha kila kitu, Mwenye hikima. Na Sisi tunakunywesheni kutokana na baadhi ya viliomo matumboni mwa hao wanyama vilio zidi katika chakula na damu maziwa safi, matamu, mepesi kuyapata kwa wanao kunywa. Katika viwele vya wanyama wa mifugo imo namna ya mitoki (glands) ambayo inachuja maziwa. Mitoki hiyo inanyweshwa na mishipa inayo leta madda maalumu kutokana na damu, na (chyle), hicho ni chakula kilicho tayarishwa. Viwili hivyo huwa vimekwisha lainishwa kwa kumezwa kama ni chakula. Kisha hapo hizo glands za maziwa huteuwa sehemu yenye kuhitajiwa kwa kufanya maziwa kutokana na vitu viwili hivyo, damu na chyle, na humiminiwa maji maalumu kugeuza hivyo vikawa maziwa yenye kukhitalifiana na asili yake kwa rangi na utamu kabisa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa
- Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu -
- Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
- Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.
- Enyi waja wangu mlio amini! Kwa hakika ardhi yangu ina wasaa. Basi niabuduni Mimi peke
- (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye
- Zilizo tiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu wengineo.
- Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na
- Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwa wakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada
- Na kwa nini tusimuamini Mwenyezi Mungu na Haki iliyo tujia, na hali tunatumai Mola wetu
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers