Surah Nisa aya 83 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا﴾
[ النساء: 83]
Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when there comes to them information about [public] security or fear, they spread it around. But if they had referred it back to the Messenger or to those of authority among them, then the ones who [can] draw correct conclusions from it would have known about it. And if not for the favor of Allah upon you and His mercy, you would have followed Satan, except for a few.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shetani ila wachache wenu tu.
Na hichi kikundi cha wanaafiki kikipata khabari zozote zilio khusu nguvu au udhaifu wa Waislamu huzitangaza na kuzieneza nje, ili kuwababaisha Waislamu au kuwatia khofu katika nyoyo zao, au ili zifike khabari zao kwa maadui wao. Na lau kuwa hawa wanaafiki watangazao wamerudisha jambo lilio kuhusu usalama au kitisho kwa Mtume na kwa wakuu wa mambo miongoni mwa waongozi na Masahaba wakubwa, wakataka kwao kujua hakika, wangeli jua hao wanao jitahidi kuchungua mambo na kuyatangaza, kuwa yaliyo kweli yanatokana na Mtume na waongozi wengine. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu kwa alivyo zithibitisha nyoyo zenu juu ya Imani, na kuzuia fitina, na rehema yake kwa kukupeni sababu na njia za ushindi, wengi wenu wangeli fuata upotovu wa Shetani, na wasingeli okoka kutokana na upotovu wake ila wachache tu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na
- Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
- Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
- Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini,
- Yeye ndiye aliye watoa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu katika nyumba zao wakati
- Basi mtayakumbuka ninayo kuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja
- Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
- Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
- Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.
- Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers