Surah Yunus aya 92 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ﴾
[ يونس: 92]
Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So today We will save you in body that you may be to those who succeed you a sign. And indeed, many among the people, of Our signs, are heedless
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.
Na leo siku ulipo angamia tutautoa mwili wako baharini, na tutauweka uwe ni onyo na funzo kwa hao walio kuwa wakikuabudu, na hawakuwa wakikutarajia utapata mwisho huu wa hizaya wa machungu. Lakini watu wengi wanaghafilika na Ishara zilizo wazi na zilizo zagaa katika ulimwengu, na ambazo zinathibitisha uwezo wetu. Inaonyesha Aya hii tukufu kuwa mwili wa Firauni utabaki umehifadhiwa ili watu wauone, na wapime kwa macho yao hali ya ule mzoga wa yule aliye kuwa akijiona ni mungu, na akiwaambia watu wake wanao mnyenyekea: Hamna mungu ila mimi! Kadhaalika tujue kuwa kutoka Wana wa Israili katika nchi ya Misri kulikuwa mwishoni mwa karne ya kumi na tatu kabla ya kuzaliwa Nabii Isa a.s., katika enzi ya mmoja wa Mafirauni wa Ukoo wa kumi na tisa, naye ni Minfitah mwana wa Ramsis wa Pili, ambaye ndiye aliye wakandamiza Wana wa Israili akawalazimisha wamjengee Jiji la ufalme wake. Uvumbuzi wa machimbo ya vitu vya kale wa hivi karibuni umedhihirisha kuwa jina la mji huo ulio funikika chini ya ardhi, ni -Buramsis-. Kulikuwa kutoka kwa Wana wa Israili pamoja na Musa ni kwa ajili ya wito wa Tawhidi, Umoja wa Mwenyezi Mungu, na kuikata shemere ya Firauni iliyo wadhalilisha, na ikawakutisha adhabu ya mwisho. Na ilikuwa haijuulikani na Waarabu ambao hawajui kusoma na kuandika, wala kwa wengineo, kwamba mwili wa Firauni huyu ungalipo mpaka hii leo. Lakini Qurani imeyataja hayo, na ukweli wake umethibiti mwaka 1900 B.K., yaani karne kumi na tatu baada ya kuteremka Qurani. Je, hii si dalili ya kuwa imetoka kwa Mungu?
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi
- Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli
- Na alipo sema Ibrahim: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyo fufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema:
- Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi,
- Wala rafiki wa dhati.
- Kisha walio dhulumu wataambiwa: Onjeni adhabu ya kudumu. Kwani mtalipwa isipo kuwa yale mliyo kuwa
- Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa
- Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia
- Ni vyake viliomo mbinguni, na viliomo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.
- Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyo itolea idhini Mwenyezi Mungu? Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers