Surah Al Imran aya 123 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾
[ آل عمران: 123]
Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And already had Allah given you victory at [the battle of] Badr while you were few in number. Then fear Allah; perhaps you will be grateful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.
Mwenyezi Mungu amewakumbusha Waumini ile neema ya nusura aliyo wapa katika vita vya Badri waliposubiri. Akawahakikishia kuwa Yeye ndiye aliye wapa ushindi katika vita vile na ingawa walikuwa wachache na wapungufu wa silaha; akawataka wamtii kuwa ni shukrani kwa neema hiyo. Badri ipo mwendo wa kiasi ya maili 120 kusini magharibi ya Madina. Mpambano hapo baina ya Waislamu na Makureshi ulikuwa siku ya Jumaane 17 Ramadhani mwaka wa pili wa Hijra (13 Machi 624 B.K.). Mtume s.a.w. na Masahaba wake walitoka Madina taarikh 8-9 ya Ramadhani mwaka wa pili wa Hijra (5 Machi 624 B.K.) Idadi ya wapiganaji wa Kiislamu katika vita hivi ilikuwa kiasi watu mia tatu au zaidi kidogo, na Washirikina walizidi mara tatu kuliko hao. Mwenyezi Mungu alitimiza ahadi yake katika vita hivi, Waumini wakashinda juu ya kuwa ni wachache, kwa kuwa Imani yao juu ya haki na uadilifu ilikuwa kubwa. Na kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa na moyo wenyewe kulikuwa ni sababu za ushindi kuliko wingi wa watu na ubora wa silaha. Ushindi huu ulio dhaahiri ukawa ndio sababu ya kuenea Neno la Imani na kutukuka likawa juu. Na hichi ni chanzo cha yaliyo kuja baadae, na kivuli cha Uislamu kikatanda Arabuni kote, na kisha kwengineko ulimwenguni.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku
- Na kama wakigeuka basi Mwenyezi Mungu anawajua waharibifu.
- Kwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Hao
- Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi,
- Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mji Mwonyaji.
- Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni
- Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono yenu, na hakika Mwenyezi
- Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?
- Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka,
- (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers