Surah Araf aya 176 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴾
[ الأعراف: 176]
Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And if We had willed, we could have elevated him thereby, but he adhered [instead] to the earth and followed his own desire. So his example is like that of the dog: if you chase him, he pants, or if you leave him, he [still] pants. That is the example of the people who denied Our signs. So relate the stories that perhaps they will give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
Na lau tungeli taka kumnyanyua afike daraja za watu wema, tungeli mnyanyua kwa kumwezesha kuyatenda maamrisho ya hizo Aya.. Lakini yeye alishikamana na dunia, na hakuweza kunyanyuka kwendea uwingu wa uwongofu. Akafuata matamanio yake. Akawa hali yake daima yumo katika dhiki, na kushughulika kwake ni kwa dunia, na tafakuri zake duniani ni kutaka kuipata hiyo dunia basi. Hali yake ni kama hali ya mbwa anapo kuwa katika hali ovu kabisa, anavyo kuwa daima anapumua na kutoa limi lake nje, ukimkemea au ukimwacha. Hudorora ulimi wake kwa kuvuta pumzi kwa shida! Kadhaalika mwenye kuipenda dunia hudumu daima katika kuwania starehe zake na matamanio yake! Hakika hizo ndizo sifa zinazo mueleza huyo mwenye kuziacha Aya zetu, na ndio sifa ya wote wanao zikadhibisha Aya zetu zilio teremka. Basi wasimulie kisa chake hichi, huenda wakafikiri na wakaamini.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Sema: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuwawa, na hata hivyo hamtastareheshwa ila kidogo
- Ufalme wa mbingu na ardhi ni wake. Na mambo yote yanarejeshwa kwa Mwenyezi Mungu.
- Je! Wana maradhi katika nyoyo zao, au wanaona shaka, au wanaogopa ya kuwa Mwenyezi Mungu
- Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili
- Je, lipo wanalo lingojea isipo kuwa matokeo yake? Siku yatapo fika matokeo yake watasema wale
- Basi kuleni katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, ikiwa mnaziamini Aya zake.
- Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu
- Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
- Walio kuwa kabla yao walikadhibisha, na ikawajia adhabu kutoka pahala wasipo patambua.
- Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye A'rshi. Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers