Surah Araf aya 133 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴾
[ الأعراف: 133]
Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali mbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wakosefu.
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So We sent upon them the flood and locusts and lice and frogs and blood as distinct signs, but they were arrogant and were a criminal people.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi tukawapelekea tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, kuwa ni Ishara mbali mbali. Nao wakapanda kiburi, na wakawa watu wakosefu.
Basi Mwenyezi Mungu aliwateremshia masaibu na balaa zaidi, kama tufani lilio funika mwahala mwao, na nzige walio kula kila mmea na mti ulio bakia, na chawa, yaani vijidudu vinavyo haribu matunda na kuteketeza wanyama na mimea. na vyura vilivyo enea vikafanya maisha yao dhiki, na vikachafua kila pahala, na damu iliyo sabibisha maradhi mengi, kama kupasuka mishipa ya damu katika mwili, na damu inayo najisisha kila pahala ikasabibisha presha, au kupasuka ikaleta kiharusi na kupooza, na kutokwa na mkojo wa damu kwa sababu ya kichocho na mfano wake, au ikawa inachanganyika na maji yao wanayo hitajia kunywa au kupikia. Mwenyezi Mungu aliwapatiliza na Ishara hizi zote zilio wazi! Nao wasiathirike, nyoyo zao zikabaki kuwa ngumu, na wenye kutakabari hawataki Imani wala kurejea kwenye Haki. Walikuwa watu walio bobea kwenye madhambi na ukosefu, kama ilivyo ada yao.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakuzaa wala hakuzaliwa.
- Na bila ya shaka tumewaelezea watu katika hii Qur'ani kila namna ya mfano. Lakini mwanaadamu
- Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao.
- Na kutoka kwa wale walio sema: Sisi ni Manasara, tulichukua ahadi yao, lakini wakasahau sehemu
- Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili
- Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni?
- Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini.
- Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na
- Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono
- Na mwezi utapo patwa,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



