Surah Maidah aya 38 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾
[ المائدة: 38]
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[As for] the thief, the male and the female, amputate their hands in recompense for what they committed as a deterrent [punishment] from Allah. And Allah is Exalted in Might and Wise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Na mwanamume aliye iba, na mwanamke aliye iba, ikateni mikono yao kuwa ni malipo ya madhambi waliyo yatenda, na njia ya kuwaonya wenginewe wasitende jambo hilo. Hiyo ni hukumu ya Mwenyezi Mungu, na amri ya Mwenyezi Mungu ndiyo yenye kushinda, naye ndiye Mwenye hikima katika kutunga Sharia. Kila ukhalifu ameuwekea malipo yake, yenye kumzuia mtu asitende tena na wengine watahadhari wasifanye kama hayo. (Ajabu iliopo ni kuwepo wajinga wakashtushwa na amri hii ya Mwenyezi Mungu aliye tuumba, na wasiseme lolote kuwa katika China wakati wa vita na Taiwan ilikuwapo sharia ya kuwa mwizi auwawe, na katika baadhi ya wilaya za Amerika mpaka hii leo ipo sharia ya kuwa mwizi wa farasi auwawe, na katika Kenya adabu ya wizi wa kutumia nguvu ni kunyongwa, na katika sharia za Kiingereza na nchi zote za magharibi mtu ana haki ya kuuwa kwa ajili ya kulinda mali na roho. Ikiwa ni haki ya mtu kumuuwa atakaye kuja kwiba, jee ni kuu hilo kwa serikali kumkata mkono aliye kwisha iba?) Kwa kuwepo sharia kama hii ndiyo ikawa wizi umetoweka katika nchi kama Saudi Arabia, na ukawa vururu kwengineko.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe yale
- Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri,
- Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
- Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta
- Kwa kitu gani amemuumba?
- Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema.
- Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo
- Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao
- Basi zitawapotea khabari siku hiyo, nao hawataulizana.
- Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers