Surah Yusuf aya 4 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ﴾
[ يوسف: 4]
Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.
Surah Yusuf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[Of these stories mention] when Joseph said to his father, "O my father, indeed I have seen [in a dream] eleven stars and the sun and the moon; I saw them prostrating to me."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.
Katika visa hivi, ewe Nabii, kipo hichi kisa cha Yusuf, pale alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeona usingizini nyota hidaAshara, (kumi na moja) na jua, na mwezi. Nimeona vyote hivyo vikininyenyekea, vikisujudu mbele yangu. Yusuf, Alayhi Ssalam, alikuwa mwana wa Yaaqub, Muabrani, Mkanaani. Akauzwa Misri katika enzi ya utawala wa wavamizi wa kigeni waitwao Wahiksos. Na kwa ionekanavyo hao Wahiksos ni katika kabila za Kisami walio ingia Misri kutoka Sham wakaiteka Delta ya Misri mnamo mwaka 1730 k.k. ( kabla ya Nabii Isa a.s.) na kabla ya kumalizika enzi ya ukoo wa kumi na tatu wa Mafirauni. Wakaihukumu Misri kwa muda wa karne unusu. Wakafukuzwa mnamo mwaka 1580 k.k. na Ahmas wa Mwanzo aliye anzisha ukoo wa 18. Wakatolewa nje ya mipaka ya Misri.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema
- Yeye ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na anafisha. Na Yeye ni Mwenye
- Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia
- Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
- Na wakubwa katika watu wake walio kufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera, na tukawadekeza kwa
- Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhaalika walio kabla yao walikanusha
- Ama walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko
- Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi
- Na Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyo kuhadithia zamani. Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe.
- Na wanayo yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao husamehe,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yusuf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yusuf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yusuf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers