Surah Tawbah aya 40 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗ وَكَلِمَةُ اللَّهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾
[ التوبة: 40]
Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
If you do not aid the Prophet - Allah has already aided him when those who disbelieved had driven him out [of Makkah] as one of two, when they were in the cave and he said to his companion, "Do not grieve; indeed Allah is with us." And Allah sent down his tranquillity upon him and supported him with angels you did not see and made the word of those who disbelieved the lowest, while the word of Allah - that is the highest. And Allah is Exalted in Might and Wise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima.
Enyi Waumini! Ikiwa nyinyi hamtasaidia kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi. Kwani Mwenyezi Mungu anatosha Yeye kumnusuru. Kama pale alipo msaidia na akamnusuru alipo tolewa Makka kwa kahari na makafiri, naye hana mwenziwe ila Abu Bakar peke yake. Wakawa wao wawili pangoni wanajificha wasionekane na washirikina walio kuwa wanawasaka wawaadhibu na kuwauwa. Abu Bakar akawa anamkhofia Mtume maisha yake. Mtume akamwambia kumpoza: Usihuzunike! Kwani hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, kwa kutunusuru na kutusaidia. Hapo Mwenyezi Mungu akamteremshia Abu Bakar utulivu, na akamuunga mkono Mtume kwa askari walio toka kwake, na ambao hawawajui ila Yeye Subhanahu. Na mambo yakamalizikia kuwa shari ya washirikina ikavia na Dini ya Mwenyezi Mungu ikashinda. Na Mwenyezi Mungu anasifika kuwa ni Mwenye nguvu, hashindiki, ni Mwenye hikima hapotei katika mipango yake. Hilo pango alilo jificha Nabii s.a.w. na rafiki yake Abu Bakar r.a. lilikuwa katika mlima wa Thor, karibu na Makka. Wakakaa humo siku tatu, baadae wakatoka usiku walipoona msako umetulia. Walifika Madina taarikh 8 katika Mwezi Rabiiul awwal (Mfungo Sita) mwaka wa kwanza wa Hijra. (20 Septemba, 630 kwa taarikh za Kizungu.)
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na
- Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa
- Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu
- Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili wawili, dume
- Ngoja tu, na wao wangoje pia.
- Na ambao wanazihifadhi Sala zao.
- Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu..
- Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu tu, na
- Na wasomee khabari za wana wawili wa Adam kwa kweli. Walipo toa mhanga, ukakubaliwa wa
- Madaraka yangu yamenipotea.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



