Surah Anfal aya 60 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ﴾
[ الأنفال: 60]
Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And prepare against them whatever you are able of power and of steeds of war by which you may terrify the enemy of Allah and your enemy and others besides them whom you do not know [but] whom Allah knows. And whatever you spend in the cause of Allah will be fully repaid to you, and you will not be wronged.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.
Enyi Umma wa Kiislamu! Tayarisheni kila muwezavyo nguvu za vita za namna zote kwa ajili ya kujizatiti kwa ajili ya kupigana, na wekeni askari walinzi na farasi wao mipakani na kando kando ya nchi, ili kwa hivi mjitayarishe na ulinzi mwatie kiwewe adui za Mwenyezi Mungu na adui zenu miongoni mwa hao makafiri ambao wamo kungojea likupateni jambo. Na pia mpate kuwatishia wenginewe ambao nyinyi hamwajui hivi sasa, lakini Mwenyezi Mungu anawajua, kwani hapana jambo linalo jificha kwake. Na kila mnacho kitoa kwa kuzitayarisha nguvu zenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi Yeye atakulipeni malipo ya kutosha, bila ya kupunguka hata chembe katika mnayo stahiki katika fadhila ya Mola wenu Mlezi Katika Aya hii tukufu pana kuhimizwa na kuamrishwa kujitayarisha kwa ajili ya kupambana na adui. Kwani vita, zamani na sasa, ni jambo la khatari na muhimu kabisa. Juu yake inategemea kheri na shari, kufa kupona kwa umati na umati. Basi yapasa kujitayarisha, kujizatiti, na kujitengeneza kwa jiha mbali mbali za vifaa na silaha na zana. Kuingia vitani bila ya kujipatia zana zote na kujitayarisha ni kutafuta kushindwa. Na tunaona hivi sasa madola yanavyo jiandaa wakati wa amani na vita, na yanavyo jenga siasa zao na mipango yao na wanavyo kusanya uwezekano wao wote ili wapate ushindi katika vita. Na vita sasa havimsazi mtu. Wanashiriki katika vita wanajeshi na raia. Kwa hivyo ndio inapasa zaidi kujitengeneza kila mmoja wao kwa matengenezo ya kuwakusanya na kuwaweka tayari wote ili upatikane ushindi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao si katika nyinyi.
- Na waache kwa muda.
- Sema: Je! Mwaonaje zile riziki alizo kuteremshieni Mwenyezi Mungu, nanyi mkafanya katika hizo nyengine haramu
- Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa,
- Na watapo hojiana huko Motoni, wanyonge watawaambia walio jitukuza: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi
- Na Thamudi hakuwabakisha,
- Na walio kufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu humo milele.
- Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
- Hatukukunjulia kifua chako?
- Wewe si mwenye kuwatawalia.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers