Surah Al Imran aya 64 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ﴾
[ آل عمران: 64]
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Say, "O People of the Scripture, come to a word that is equitable between us and you - that we will not worship except Allah and not associate anything with Him and not take one another as lords instead of Allah." But if they turn away, then say, "Bear witness that we are Muslims [submitting to Him]."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu.
Sema, ewe Nabii! Enyi Watu wa Kitabu! (Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo) njooni kwenye neno moja la uadilifu lenye kutukusanya sote na tunalo litaja, nalo ni kuwa hatumuabudu ila Mwenyezi Mungu tu, wala tusimwekee washirika katika ibada. Na wala tusiwe tunawatii baadhi yetu tukiwafuata katika kuhalalisha na kuharimisha, tukaachilia mbali hukumu ya Mwenyezi Mungu katika mambo ya halali na haramu. Wakiukataa wito huu wa haki waambie: Shuhudieni kuwa sisi ni Waislamu, yaani tunafuata hukumu za Mwenyezi Mungu, na Yeye tu tumemsafia Dini, wala hatumwombi mwengineyo. (Taurati:Kutoka 20.3:Usiwe na miungu mingine ila Mimi. Injili ya Marko 12.29 : Yesu akamjibu, [amri] Ya kwanza ndiyo hii, Sikia Israel, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole.
- Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.
- Pale walio kufuru walipo tia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha
- Harun, ndugu yangu.
- Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha
- Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo
- Mfano wa vile wanavyo vitoa katika uhai wao wa duniani ni kama upepo ambao ndani
- Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers