Surah Mumtahina aya 4 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴾
[ الممتحنة: 4]
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.
Surah Al-Mumtahanah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
There has already been for you an excellent pattern in Abraham and those with him, when they said to their people, "Indeed, we are disassociated from you and from whatever you worship other than Allah. We have denied you, and there has appeared between us and you animosity and hatred forever until you believe in Allah alone" except for the saying of Abraham to his father, "I will surely ask forgiveness for you, but I have not [power to do] for you anything against Allah. Our Lord, upon You we have relied, and to You we have returned, and to You is the destination.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.
Nyinyi mna kiigizo kizuri cha kukiiga katika Ibrahim na walio amini pamoja naye, pale walipo waambia watu wao: Hakika sisi tunajitenga nanyi, na tunajitenga na hiyo miungu ya uwongo mnayo iabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Sisi tunakukataeni, na umekwisha dhihiri uadui na kuchukiana baina yetu na nyinyi. Hayo hayataondoka kabisa mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake. Lakini kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Nitakutakia maghfira, na similiki kwa Mwenyezi Mungu kitu chochote - kauli hiyo si ya kufuatwa. Kwani hayo yalikuwa kabla hajajua huyo baba yake kashikilia kuwa adui wa Mwenyezi Mungu wala hageuki. Ilipo dhihiri kwake kuwa hakika huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu alijitenga naye. Enyi waumini! Semeni: Mola wetu Mlezi! Kwako Wewe ndio tunategemea, na kwako Wewe tunarejea, na kwako Wewe ndio mwisho wetu Akhera.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wala usivikodolee macho tulivyo wastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya
- Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, ila kwa sababu ya kuwajaribu tujue nani
- Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tunafuata tuliyo wakuta nayo baba
- Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa.
- Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
- Tulimwita: Ewe Ibrahim!
- Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.
- Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa
- Na Ismail, na Al Yasaa, na Yunus, na Lut'. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu
- Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Mumtahina with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Mumtahina mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Mumtahina Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers