Surah Fussilat aya 9 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴾
[ فصلت: 9]
Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Surah Fussilat in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Say, "Do you indeed disbelieve in He who created the earth in two days and attribute to Him equals? That is the Lord of the worlds."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Ewe Mtume! Waambie hawa washirikina: Ama nyinyi mnastaajabisha! Mnamkataa Mwenyezi Mungu aliye iumba ardhi kwa siku mbili, na huku juu ya hayo, mnamfanyia washirika wa kushirikiana naye huyo Muumba ardhi, Mmiliki wa walimwengu wote na Mlezi wao? Zimetajwa Siku moja au Siku nyingi katika Sura nyengine. Katika Surat Al-Hajj, Aya 47 Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: -Na kwa hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyo hisabu nyinyi.- Na katika Surat Assajdah, Aya 5 amesema Mtukufu: -Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni miaka elfu mnayo hisabu.- Na katika Surat Al-Maarij Mtukufu amesema: -Malaika na Roho hupanda kwake katika siku iliyo kadiri yake ni miaka elfu khamsini.- Maoni ya kitaalamu: Vipimo vya wakati wanavyo vitumia watu vimefungamana na dunia na inavyo zunguka juu ya msumari-kati wake na kulizunguka jua. Mtu akitoka kwenye ardhi (dunia) akenda kwenye sayari nyengine za mbinguni vipimo hivyo vya nyakati vinabadilika kwa kuzidi au kwa kupungua. Na hizi Aya tukufu zinaonyesha ishara ya ukweli huu wa ki-ilimu, na ya kwamba zama au nyakati ni jambo la mlinganisho tu. Na bila ya shaka ipo miaka ya ki-ilimu ya Falaki ya kulinganisha yenye kumkinika kuifarikisha baina yao. Mwaka wa ki-jua wa duniani huhisabiwa kwa kupimwa wakati ambao dunia inachukua kulizunguka jua kwa ukamilifu mnamo siku 365, na ilhali sayari zilio karibu na jua kama Utaarid (Mercury) humaliza safari yake ya kulizunguka jua mnamo siku 88, na upande mwengine sayari ya Blutu (Pluto) ambayo ndiyo sayari iliyo mbali mno na jua, na ndiyo inazunguka taratibu mno inachukua kuzunguka kwake mnamo miaka 250 kwa mujibu wa miaka yetu sisi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Tupa fimbo yako. Mara ikavimeza vyote vile walivyo vibuni.
- Ambao unapanda nyoyoni.
- Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo.
- Na tunge utuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wange endelea
- Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
- Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur'ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote hapana
- Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako. Na
- Hizi ni Aya za Kitabu chenye hikima.
- Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu
- Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Fussilat with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Fussilat mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Fussilat Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers