Surah Anfal aya 9 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ﴾
[ الأنفال: 9]
Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni kuwa: Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu wanao fuatana mfululizo.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[Remember] when you asked help of your Lord, and He answered you, "Indeed, I will reinforce you with a thousand from the angels, following one another."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni kuwa: Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu wanao fuatana mfululizo.
Na enyi Waumini! Kumbukeni nanyi mnagawana ngawira na mnakhitalifiana, mlipo omba uwokovu na msaada, na mkaandikiwa kuwa hapana la kukuepusheni na vita. Mwenyezi Mungu alikuitikieni maombi yenu, akakuungeni mkono kwa kukuleteeni (Malaika) Roho zilizo safi nyingi zinazo fika elfu zinazo fuatana, zikija moja baada ya moja. Walipo jua wapiganaji Waumini kuwa hapana njia ya kuepukana na vita wakaomba msaada kwa Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu Mtukufu akawaitikia, na akawaunga mkono kwa Malaika elfu walio fuatana. Yaani alianza kwa kupeleka msaada kwa vikosi vilivyo fuatana ili iwe wepesi kwa kila kikosi kuelekea pahala pake katika vita pasiwepo kukaa bure au kupigana makumbo. Na ifikapo misaada ya majeshi ya vita roho hufurahi na moyo huingia nguvu. Na hayo ndiyo aliyo yakusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kauli yake: -Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe.- Na ushindi daima unatokana na Mwenyezi Mungu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.
- Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe.
- Na ama walio amini na wakatenda mema atawalipa ujira wao sawa sawa, na atawazidishia kwa
- Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?
- Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda
- Na Manaat, mwingine wa tatu?
- Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili?
- Na wamechukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
- Na kwa masiku kumi,
- Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya walio kufuru (na watasema:)
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers