Surah Baqarah aya 104 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴾
[ البقرة: 104]
Enyi mlio amini! Msiseme: "Raa'ina", na semeni: "Ndhurna". Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, say not [to Allah 's Messenger], "Ra'ina" but say, "Unthurna" and listen. And for the disbelievers is a painful punishment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Msiseme: -Raaina-, na semeni: -Ndhurna-. Na sikieni! Na makafiri watapata adhabu chungu.
Enyi mlio amini! Tahadharini na hawa Mayahudi. Msimwambie Mtume pale anapo kusomeeni ufunuo: -Raaina- kwa kukusudia akuwekeni pahala pa uangalizi wake, yaani (Tuchunge, Turai), na akupeni muda katika kusoma kwake mpaka mzingatie na mhifadhi. Kwani watu makhabithi miongoni mwa Mayahudi husaidiana kutaka kukuigeni na kupindua ndimi zao kwa neno hilo mpaka likawa neno la matusi wanalo lijua wao. Na wao humkabili Mtume kwa neno hilo kwa kumfanyia maskhara. Lakini nyinyi tumieni neno jingine wasilo weza Mayahudi kulipatia njia ya kufanya ukhabithi wao na maskhara yao. Tumieni neno: -Ndhurna- yaani -Tuangalie-. Na sikilizeni vyema anayo kusomeeni Mtume. Na Mwenyezi Mungu anawadundulizia adhabu kali kwa Siku ya Kiyama hawa wanao mfanyia maskhara Mtume. Katika lugha ya Kiyahudi ya Kiebrania lipo neno -Rainu- ambalo limejengwa na neno -Ra- kwa maana ya -Shari- na neno -nu- linaonesha jamii, wingi. Na maana ya neno lote ni kuwa -Wewe ni shari yetu-, wakikusudia kumwambia Mtume hayo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.
- Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye
- Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
- Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.
- Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni
- Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo
- Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani?
- Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
- Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
- Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers