Surah Mulk aya 19 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ﴾
[ الملك: 19]
Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyo zikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.
Surah Al-Mulk in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Do they not see the birds above them with wings outspread and [sometimes] folded in? None holds them [aloft] except the Most Merciful. Indeed He is, of all things, Seeing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyo zikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.
Wameingia upofu? Wala hawakuwaangalia ndege walio juu yao, vipi wanavyo kunjua mbawa zao mara kwa mara, na mara nyingine wakizikunja? Hapana anaye washikilia wasianguke ila Mwingi wa Rehema. Hakika Yeye ni Mwingi wa ujuzi na khabari kwa kila kitu. Anakipa kila kitu jambo kwa mujibu wa maslaha yake. Kukunjua huku ni kukunjua ndege mbawa zake bila ya kuziendesha. Katika kuruka kwa ndege ipo miujiza ambayo haikufahamika baadhi yake ila baada ya kuendelea ilimu ya kuruka na nadhariya ya kutembea katika hewa. Lakini katika yanayo staajabisha ni kupita ndege katika anga na mbawa zote mbili zimetulia mpaka apite upeo wa macho. Na ilimu imevumbua kuwa ndege wanao kunjua mbawa zao hupanda juu ya mikondo ya hewa inayo saidia inayo timbuka ama kwa kupigana dafrau na kiziwizi fulani au kwa kunyanyuka nguzo za hewa imoto. Ukiwa upepo ni mzuri hizo nguzo za hewa husimama wima na ndege hupaa kwa namna ya mzunguko kama skurubu. Na ukiwa mkali hizo nguzo hugeuka kuelekea juu na ndege huruka bila ya kupiga mbawa kwa njia ya sawa moja kwa moja na kufikia mbali. Na ndege kwa jumla wana sifa maalumu, katika hizo ni kuwa ni wepesi, na wana umbo la nguvu, na nyoyo zao ni madhubuti, na kadhaalika mzunguko wao wa damu, na vyombo vya kuvutia pumzi, na namna lilivyo pimika umbo lao, na vikawa sawa sawa viwiliwili vyao kwa kusahilisha kuruka katika hewa. Na sifa hizi Mwenyezi Mungu Mjuzi Mwenye kuona kawajaalia ndege , kwa ajili ya kuwahifadhi hao ndege katika hewa pale wanapo kunjua mbawa zao au wanapo zikunja. Ama videge vidogo vinavyo tegemea kuruka kwao juu ya mbio, hivyo hupiga mbawa zao kwa chini na mbele ili vipate kujisukuma na kupaa. Na hayo ni dharura kwa sababu ya kuruka kwao. Kisha huzikunja mbawa zao, lakini nao wanabaki kuwa wanaruka kwa zile nguvu za msukumo wao. Na hivyo linawafikiana umbo lao hao ndege wa kila namna na muundo wa kifundi wa miili yao kwa kuwazesha kuruka na kujilinda sawa wakati wa kuruka.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makaazi ya
- Wakasema wale wanao jivuna: Sisi tunayakataa hayo mnayo yaamini.
- Walio sema: Mwenyezi Mungu ametuahidi tusimuamini Mtume yeyote mpaka atuletee kafara inayo teketezwa na moto.
- Yule ambaye Mwenyezi Mungu amemhidi basi huyo amehidika; na alio waacha kupotea basi hao ndio
- (Wajumbe) wakasema: Ewe Lut'! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa hawatakufikia. Na wewe
- Na katika hao mnayo manufaa kadhaa wa kadhaa, na mnapata kwao haja ziliomo vifuani mwenu;
- Sema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingi wa Rahema atawapururia muda mpaka wayaone waliyo onywa
- Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo.
- Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
- Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Mulk with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Mulk mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Mulk Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers