Surah Raad aya 26 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿اللَّهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ وَفَرِحُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ﴾
[ الرعد: 26]
Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah extends provision for whom He wills and restricts [it]. And they rejoice in the worldly life, while the worldly life is not, compared to the Hereafter, except [brief] enjoyment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo.
Na ikiwa hao washirikina wanaona kuwa wao wamepewa mali mengi, na Waumini ni mafakiri, wanyonge, basi wajue kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humpa riziki kunjufu amtakaye akizishika sababu na humdhikisha amtakaye. Basi Yeye humpa Muumini na asiye kuwa Muumini. Kwa hivyo msidhani kuwa wingi wa mali mikononi mwao kuwa ni dalili ya kuwa wao ndio wamo katika Haki. Lakini wao hufurahi kwa hayo mali walio pewa, juu ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humpa dunia anaye mpenda na asiye mpenda. Na maisha ya duniani si chochote ila ni starehe duni yenye kupita!
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wajumbe wetu walipo mfikia Lut'i, alihuzunika kwa ajili yao, na moyo uliona dhiki kwa
- Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali mnajua?
- Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala
- Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho?
- Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia
- Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa
- Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
- Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale walio kuwa wanataka maisha ya duniani:
- Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
- Na bahari mbili haziwi sawa; haya ni matamu yenye ladha, mazuri kunywa. Na haya ni
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers