Surah Hajj aya 44 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَأَصْحَابُ مَدْيَنَ ۖ وَكُذِّبَ مُوسَىٰ فَأَمْلَيْتُ لِلْكَافِرِينَ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ﴾
[ الحج: 44]
Na watu wa Madiana. Na Musa pia alikanushwa. Nikawapa muda makafiri, kisha nikawatia mkononi. Basi ilikuwaje adhabu yangu!
Surah Al-Hajj in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And the inhabitants of Madyan. And Moses was denied, so I prolonged enjoyment for the disbelievers; then I seized them, and how [terrible] was My reproach.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na watu wa Madiana. Na Musa pia alikanushwa. Nikawapa muda makafiri, kisha nikawatia mkononi. Basi ilikuwaje adhabu yangu!
Na watu wa Madiana walimkanusha Mtume wao Shuaib. Na Firauni na watu wake walimkanusha Mtume wa Mwenyezi Mungu Musa. Mitume hao wote yaliwapata yanayo kupata wewe. Na Mimi niliwapa muhula hao wakanushao ili wapate kutubia waongoke, na waitikie Wito wa Haki. Lakini wakazua na wakaendelea na kuwakadhibisha Mitume wao na kuwaudhi. Wakazidisha madhambi juu ya madhambi yao. Basi nikawaadhibu ukomo wa kuwaadhibu. Angalia taarikhi yao utaona kuwa adhabu yangu ilikuwa kali mno, pale nilipo ibadilisha neema ikawa nakama, na uzima ukawa ni maangamizo, na badala ya ujenzi ukawa uharibifu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko
- Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?
- Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipo kuwa tuliye mkuta naye kitu chetu.
- Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na
- Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?
- Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu.
- Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
- Na walio shirikisha watakapo waona hao walio washirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: Mola wetu Mlezi!
- Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.
- Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hajj with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hajj mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hajj Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



