Surah Anfal aya 57 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ﴾
[ الأنفال: 57]
Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So if you, [O Muhammad], gain dominance over them in war, disperse by [means of] them those behind them that perhaps they will be reminded.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.
Basi ewe Mtume! Ukiwakuta hawa wavunjao mapatano, na ukasadifiana nao katika vita nawe umeshinda, basi watishe baraabara kwa kuwapa adhabu ya kuwatia uchungu na kuwaogopesha wale walio nyuma yao, upate kuwafarikisha walio baki. Mateso haya ndiyo ya kuwakumbusha uovu wa kuvunja mapatano, na kuwazuia wenginewe wasitende kama hayo. Katika Aya tukufu hizi tunahadharishwa na wale wanao toa ahadi na kisha wakazivunja. Hawa yafaa wapewe adhabu ya kutia mfano kwao na kwa walio nyuma yao. Na katika Aya hii unabainishwa umuhimu wa kuvuruga askari wa adui walio nyuma. Hizi ni mbinu za vita za kisasa, kwani kuzua vurugo katika askari wa nyuma hutosha kuleta fujo na kupelekea jeshi kutawanya askari wake kulinda mgongo wake, na kwa hivyo zinavunjika nguvu zake. Juu ya hivyo katika sehemu za nyuma katika midani ndio huwapo mambo yaliyo khusu idara ya jeshi ambayo juu yake ndio jeshi linategemea kwa msaada. Ukileta vurugu hapa hupelekea kukosekana nidhamu yote ya jeshi, na kwa hivyo ndio huleta kuemewa na kushindwa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha
- Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati
- Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya
- Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
- Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipo dhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.
- Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
- Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
- Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina a'mali yangu, na nyinyi mna a'mali yenu. Nyinyi hamna
- Na tumeacha katika mji huo Ishara ilio wazi kwa watu wanao tumia akili zao.
- Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers