Surah Qasas aya 73 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾
[ القصص: 73]
Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.
Surah Al-Qasas in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And out of His mercy He made for you the night and the day that you may rest therein and [by day] seek from His bounty and [that] perhaps you will be grateful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.
Na miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake ni kuwa kawaumbia usiku na mchana, inayo fuatana, ili wapate kupumzika usiku, na washughulikie kutafuta riziki zao na manufaa yao mengine wakati wa mchana, na watambue fadhila za Mwenyezi Mungu juu yao wapate kumshukuru. -Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni mwangaza? Basi je, hamsikii? Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku mkapumzika humo? Basi je, hamwoni? Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.- Hapana shaka kuwa kuumbwa kwa dunia kwa namna yake ilivyo sasa na ilivyo wekwa kwa mnasaba wa jua, na kuzunguka kwake wenyewe kwa wenyewe kila siku, na kulizunguka jua kila mwaka, hapana shaka kwamba haya yanaonyesha dhaahiri uwezo wa Mwenyezi Mungu na upweke wake. Na Aya tukufu inawazindua watu watambue ukweli ambao yawapasa wauelewe, nao ni kwamba Yeye Mtukufu lau kuwa aliumba dunia iwe na usiku wa milele, au iwe na mchana wa milele, basi hapanapo mungu mwengine anaye weza kuwaneemesha watu kwa mchana na usiku wa kufuatana kama hivi. Na hivyo ni kuwa lau kuwa dunia inazunguka juu ya msumari-kati wake na pia kulizunguka jua kwa kiwango kimoja kiasi ya siku 365 takriban, yangeli tokea mabadiliko makubwa mno. Miongoni mwao ni kudumu giza katika nusu ya dunia, na kudumu mwangaza katika nusu ya pili takriban. Na kwa hivi joto lingeli panda katika nusu yenye mwangaza kwa kiasi kisicho weza kuchukulika. Na nusu yenye giza ingeganda kwa barafu. Na pande zote mbili zisingeweza kuchukua kitu chochote chenye uhai. Ama huu mpango ulivyo sasa unapelekea kupishana usiku na mchana, na kwa hivyo kunapatikana mapumziko na utulivu wakati wa usiku, na kushughulika wakati wa mchana. Na hali ya hewa inasilihi uhai wa binaadamu, na wanyama, na mimea. Na haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, ambazo zinapelekea tukubali uwezo wake, na tudumu kumshukuru.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kwa hakika wanaume wanao toa sadaka, na wanawake wanao toa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu
- Kutokana na majini na wanaadamu.
- Hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu,
- Waombee msamaha au usiwaombee. Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa
- Basi ikauonja ubaya wa mambo yake; na mwisho wa mambo yao ilikuwa khasara.
- Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha.
- Hatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyomo baina yake ila kwa haki na kwa muda maalumu.
- Na tungeli penda tungeli yaondoa tuliyo kufunulia. Kisha usingeli pata mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa
- Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi
- Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Qasas with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Qasas mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Qasas Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers