Surah Waqiah aya 76 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ﴾
[ الواقعة: 76]
Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
Surah Al-Waqiah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And indeed, it is an oath - if you could know - [most] great.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
Na hakika bila ya shaka hicho ni kiapo kikubwa chenye maana ya kufikia mbali, lau kuwa mnafikiri makusudio yake. Aya mbili hizi zinabainisha hadi ya umuhimu wa kiapo hichi kikubwa. Kwani nyota ni vitu vyenye kutoa mwangaza wenyewe, na nyota ya karibu mno kwetu sisi, nayo ni jua, ni kiasi ya masafa ya miaka 500 ya mwangaza. Na nyota ifuatayo kwa ukaribu iko mbali nasi kwa kiasi cha miaka 4 ya mwangaza takriban. Basi nguvu tunazo zitumia kutokana na jua ndizo zinazo tuwezesha kuishi. Lau kuwa umbali wa jua kutokana na ardhi ni duni ya hivyo au zaidi ya hivyo basi hapana shaka kuwa maisha yangeli kuwa taabu, bali ni muhali. Kadhaalika ukubwa wa nyota unakhitalifiana. Zipo nyota kubwa mno hata ukubwa wake unaweza kukusanya hii ardhi na jua juu ya umbali wao. Vipo vikundi vya nyota vinavyo itwa Anaqiid vinaogelea angani zikivuka Njia ya Maziwa The Milky Way mara kwa mara. Wakati wa kupita kwake zikasadifiana kukutana na kikundi cha jua na zikagongana basi hakika hapo itakuwa ndio maangamizo na kumalizika kwa kweli. Hata ikikaribia nyota moja katika nyota zitokazo kwenye jua basi hayo pia yataleta kuharibika mizani na kupelekea maangamizo na kumalizika ulimwengu. Kwa hivyo basi hakika Ishara za mazingatio na uweza wa Mwenyezi Mungu zinaonekana katika ulimwengu huu alio uumba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na akaupanga.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na
- Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
- Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je,
- Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate
- Naapa kwa tini na zaituni!
- Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizo zifanya. Na adhabu mbaya itawazunguka watu
- Yeye ndiye Mwenye kujua yanayo onekana na yasio onekana; Mkuu Aliye tukuka.
- Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
- Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi
- Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Waqiah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Waqiah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Waqiah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



