Surah Yusuf aya 96 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَلَمَّا أَن جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴾
[ يوسف: 96]
Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona. Akasema: Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi?
Surah Yusuf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when the bearer of good tidings arrived, he cast it over his face, and he returned [once again] seeing. He said, "Did I not tell you that I know from Allah that which you do not know?"
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona. Akasema: Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi?
Akashikilia tamaa yake akingojea rehema ya Mwenyezi Mungu, na ahali zake wakashikilia kumdhania dhana mbovu mpaka alipo fika mtu aliye chukua kanzu na kumbashiria kwamba Yusuf yupo salama salmina. Ilipo wekwa kanzu usoni kwa Yaaqub akainusa harufu yake, moyo wake ulijaa furaha, macho yake yakarejea kuona. Yule mjumbe alipo msimulia hali ya Yusuf, na kwamba anamtaka yeye asafiri ende pamoja na ahali zake, aliwageukia walio kuwa naye akiwakumbusha ule utabiri wake, na akiwakaripia kwa vile walivyo mkadhibisha. Akawataka wakumbuke yale aliyo wahakikishia pale punde kwamba yeye anaijua rehema ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake wasio ijua wao.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
- Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora
- Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.
- Na mkakaa katika maskani zile zile za walio zidhulumu nafsi zao. Na ikakudhihirikieni jinsi tulivyo
- Hawa wagomvi wawili walio gombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi. Basi walio kufuru watakatiwa
- Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
- Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu nawe umo pamoja nao, wala Mwenyezi Mungu si wa
- Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili.
- Je, wamejiaminisha na mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Mungu ila
- Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha, anavyo somewa asubuhi na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yusuf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yusuf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yusuf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers