Surah Anfal aya 11 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ﴾
[ الأنفال: 11]
Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shet'ani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu yenu.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[Remember] when He overwhelmed you with drowsiness [giving] security from Him and sent down upon you from the sky, rain by which to purify you and remove from you the evil [suggestions] of Satan and to make steadfast your hearts and plant firmly thereby your feet.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shetani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu yenu.
Enyi Waumini! Kumbukeni wakati mlipo ingiwa khofu kwa upungufu wa maji, na kuwaogopa maadui. Mwenyezi Mungu alikupeni utulivu, kwa kukuleteeni usingizi, mkalala mkatua. Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni mkajisafishia, na mkauondoa wasiwasi wa Shetani, na nyoyo zenu zikawa imara kwa msaada wa Rahmani na pia ardhi ikashikamana kwa hayo maji, na miguu yenu ikaweza kukanyaga bila ya kudidimia katika mchanga. Aya hii inaashiria fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya wapiganaji Waumini kwa kupatikana hali ya amani kwa kupumzika kwa usingizi, na kuteremka mvua kwa kujitahirisha na kukoga, na kushikamana mchanga kwa kuwepo maji, basi nyayo zikasimama imara. Inajuulikana kuwa mchanga laini unawaletea taabu wapiganaji na unakuwa pingamizi katika kwenda huku na huko ambako ni katika dharura za vita muhimu. Na aya ya pili inaeleza maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwaambia Malaika wawathibitishe Waumini na watie khofu katika nyoyo za makafiri. Na ni maarufu kuwa khofu ikiwatawala askari katika midani huwaletea kuemewa. Na katika Aya hii tukufu panaashiriwa pahali pa kupiga napo ni juu ya shingo na kuvikata vidole vinavyo kamata silaha mkononi.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika
- (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo
- Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
- Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.
- Basi mbona wale walio washika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru?
- Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo
- Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
- Na nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu.
- Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani
- Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



