Surah Luqman aya 13 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ﴾
[ لقمان: 13]
Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa.
Surah Luqman in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [mention, O Muhammad], when Luqman said to his son while he was instructing him, "O my son, do not associate [anything] with Allah. Indeed, association [with him] is great injustice."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa.
Taja pale Luqman alipo mwambia mwanawe: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu na yeyote. Hakika kumshirikisha Mwenyezi Mungu ni dhulma kubwa, kuwaweka sawa Mwenye kustahiki na asiye stahiki. Waarabu walikuwa wanawajua watu wawili kwa jina hili. Mmoja wapo ni Luqman bin aadi. Nao walikuwa wakimtukuza cheo kwa werevu wake, uraisi, ujuzi, ufasihi na ujanja. Na walikithiri sana kumtaja na kumpigia mithali, kama inavyo onekana katika vitabu vya Kiarabu vingi. Ama mwengine ni huyo anaye itwa Luqman Alhakim, (Mwenye hikima), aliye kuwa mashuhuri kwa hikima yake na mifano yake, na ambaye Sura hii ya Qurani imeitwa kwa jina lake. Na hikima zake zilikuwa zimeenea kwa Waarabu. Ibn Hisham amesimulia kwamba Suwaid bin Assamit alifika Makka. Naye alikuwa mtu mtukufu kwa watu wake. Mtume s.a.w. akamtaka asilimu. Suwaid akasema: Huenda labda uliyo nayo wewe ndiyo kama niliyo nayo mimi. Mtume s.a.w. akasema: Nini ulicho nacho? Akasema: Majalla ya Luqman. Mtume s.a.w. akasema: Nisomee. Akamsomea. Tena akasema: Hakika haya maneno mazuri. Na niliyo nayo mimi ni bora zaidi, nayo ni Qurani aliyo niteremshia Mwenyezi Mungu, nayo ni Uwongofu na Nuru. Mtume s.a.w. akamsomea Qurani na akamtaka asilimu. Na pia Imam Malik ametaja kwa wingi hikima za Luqman katika kitabu chake, Al Muwatta. Na baadhi ya vitabu vya Tafsiri ya Qurani na Adab (maandishi ya ufasihi wa lugha) vimetaja namna mbali mbali katika hikima hizo. Kisha baadae ikakusanywa mithali kwa visa katika kitabu chenye jina la Mithali za Luqman. Lakini kwa sababu ya udhaifu wa mpango wake, na wingi wa makosa ya nahau na sarfu, na kuwa kutopokewa kitabu cha jina hili katika vitabu vya Waarabu wa kale, yatilia nguvu kuwa hichi kimezuliwa tu katika zama za mwisho. Na maoni yanayo gongana juu ya uhakika wa Luqman Al-hakim: ni kuwa yeye ni Mnubi katika watu wa Abla au Uhabeshi, au mtu mweusi wa Sudan ya Misri, au ni Muibrani. Na wengi walio mtaja wanakubaliana kuwa hakuwa Nabii. Wachache tu ndio wanasema kuwa alikuwa Nabii. Na tunalo weza kutambua katika yaliyo tajwa ni kuwa hakuwa Mwaarabu, kwa sababu wote wamewafikiana kwa hayo. Na kwamba alikuwa ni mtu mwenye hikima, na hakuwa Nabii, na kwamba ameingiza miongoni mwa Waarabu hikima mpya zikawa zinatajwa mara nyingi kama ilivyo onekana baadae katika vitabu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.
- Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika
- Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni
- Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.
- Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu
- Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
- Basi ni nani aliye dhaalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu na akazikanusha
- Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
- Basi sisi hakika tutakueletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo
- Ewe mwanangu! Shika Sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Luqman with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Luqman mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Luqman Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers