Surah Yasin aya 40 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ﴾
[ يس: 40]
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
Surah Ya-Sin in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
It is not allowable for the sun to reach the moon, nor does the night overtake the day, but each, in an orbit, is swimming.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
Haipelekei jua likaacha sharia zake likakutana na mwezi, na likaingia katika njia zake. Wala usiku hauwi kuushinda mchana ukauzuia usije, bali vyote viwili hivyo hupeana zamu. Na vyote, jua na mwezi, na vyenginevyo vyote vinaogelea katika njia zao za mbinguni, wala haviachi njia. Hakika Aya hizi tukufu zinabainisha ukweli wa ki-ilimu ambao wataalamu walikuwa hawaujui ila mwanzo wa karne ya kumi na nne ya kuzaliwa Nabii Isa. Na jua ni moja katika nyota za mbinguni, nalo kama nyota zilizo baki lina mwendo wake wenyewe. Lakini linakhitalifiana na nyota nyengine kwa kuwa lipo karibu na dunia, na kwa kuwa lina kundi la sayari na miezi ya mikia na sayari ndogo ndogo zinazo lifuata daima, na zinatii mvuto wake. Kwa hivyo zinakuwa hizo zinazunguka kwa kufuatana kwa utungo kama sura ya yai. Na mkusanyo wote huu unakwenda angani pamoja na jua kwa mvuto wake. Kwa ufupi jua, na ardhi, na mwezi na sayari zote na vyombo vyote hivyo vinakwenda angani kwa mbio maalumu, na kuelekea jiha maalumu. Na yaonekana kuwa jua na mkusanyo wote huo wake, na nyota zilizo karibu nalo zipo katika mkusanyo ulio tanda katika mbingu inayo itwa kwa Kiarabu Sadiimu almajarrah, au kwa Kiingereza Nebula course. Na imebainika kwa masomo ya kisasa sehemu zote za hiyo Nebula zinaizunguka kati yake kwa mbio ya kunasibiana na kinyume cha umbali wake kutoka hapo kati. Pia imeonakana kuwa jua na ardhi na sayari zake na nyota zilio karibu nayo, vyote hivyo vinakwenda mbio, na upande maalumu. Mbio zake zinafika kilomita 700 kila nukta moja. Na kunatimia kuzunguka kwake kukizunguka hicho kituo cha kati kwa kiasi ya miaka milioni 200 ya muangaza. Na kiini cha maneno ni kuwa Aya tukufu iliyo taja kuwa jua linakwenda kwa kiwango chake, hawakujua wataalamu uzuri wake wa ndani mpaka katika mwanzo wa karne hii. Wala hayamkini jua kuupata mwezi, kwani kila kimojapo kinakwenda katika njia zake mbali mbali, basi ni muhali kukutana, kama ilivyo kuwa ni muhali kupitana usiku na mchana. Hayo ingeli takikana ardhi izunguke juu ya msumari-kati wake kutoka mashariki kwendea magharibi, kinyume na ilivyo hivi sasa kutoka magharibi kwendea mashariki. Na mwezi katika kuizunguka kwake ardhi, na ardhi kulizunguka jua, huenda pamoja na mkusanyo wa nyota unao itwa Manaazil Alqamar au Lunar system. Na katika robo ya mwanzo na ya mwisho wa mwezi huonekana sura yake kama karara kongwe au kole lilio kauka, linapo kuwa kongwe na kunyauka.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi
- Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
- Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.
- Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
- Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio mtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na waliyo
- Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale walio wafanyia maskhara yaliwafika yale
- Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
- Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
- Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
- Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale yaliyo tangulizwa na mikono yao; na Mwenyezi Mungu
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yasin with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yasin mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yasin Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers