Surah Assaaffat aya 5 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ﴾
[ الصافات: 5]
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
Surah As-Saaffat in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Lord of the heavens and the earth and that between them and Lord of the sunrises.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
Yeye - peke yake - ndiye Muumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao, na ndiye Mwenye kupanga mambo, na ndiye Mwenye kutawala mashariki za kila chenye mashariki. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba mbingu saba na viliomo baina yao, navyo ni hivyo vyombo vya mbinguni na nyota zake. Naye ndiye Mwenye kusimamisha, Mwenye kulinda vile vile juu ya mwahali zinapo chomozea jua na nyota zote. Na Yeye ndiye anaye vionyesha hivyo kila siku katika pahala huko upeo wa macho, kila siku pahala mbali na vilipo dhihiri siku iliyo tangulia. Na hayo ni kwa mwendo wa mpango wa jua maalumu kwa inavyo zunguka dunia juu ya msumari-kati wake kutoka magharibi kwendea mashariki kila siku na wakati huo huo inavyo lizunguka jua katika njia yake katika falaki. Na jua na nyota huonekana na wakaazi wa ardhi kila siku kama zinachomoza mwahala mbali mbali. Na kila ardhi ikigeuza mahala pake katika safari yake katika mbingu linaonekana jua linachomoza pahala pengine. Ukiliangalia jua kwa utulivu kuanzia mwishoni wa mwezi wa Machi, yaani linapo kuwa jua lipo kati ya mstari wa Ikweta mwanzo wa musimu wa Rabii, yaani Spring, kwa nusu ya kaskazini ya dunia, utaliona linachomoza pahala katika mashariki juu ya upeo wa macho. Kwa mwenye kupeleleza kila siku ikipita ataona kuchomoza kwake kunajongelea kaskazini. Na mwishoni mwa mwezi wa Juni utaona linachomozea mwisho wa kukaribia kaskazini. Kisha baada ya hapo utaliona jua linarejea linafuata kugeuka kule kule mpaka mwisho wa Septemba (wakati wa kuwa sawa wakati wa Khariif yaani Autumn) utaliona jua linachomoza pale pale lilipo chomoza mwanzo wa Machi. Kisha litaendelea kuelekea kusini kuchomoza kwake mpaka mwisho wa Desemba linakuwa linachomoza karibu kabisa na kusini. Baada ya hapo huanza tena kurejea kuelekea kaskazini mpaka limalize safari yake ya kufika kati sawa katika Rabii ya pili. Na safari hii yote inachukua siku 365 na robo siku. Na inaonekana kuwa nyota nazo zinachomoza mwahala mbali mbali katika upeo wa macho inapo kuwa dunia imo katika safari yake ya mbinguni, na khasa nyota za buruji (au vituo) 12 vinavyo pitiwa na jua katika mwendo wake wa mwaka.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni
- Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na
- Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu,
- Wako juu ya viti wamekabiliana.
- Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
- (Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee
- Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila
- Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
- Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.
- Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Assaaffat with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Assaaffat mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Assaaffat Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers