La sourate Al-Maarij en Swahili
سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ(1) Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, |
لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ(2) Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - |
مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ(3) Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. |
تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ(4) Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! |
فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا(5) Basi subiri kwa subira njema. |
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا(6) Hakika wao wanaiona iko mbali, |
وَنَرَاهُ قَرِيبًا(7) Na Sisi tunaiona iko karibu. |
يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ(8) Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. |
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ(9) Na milima itakuwa kama sufi. |
وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا(10) Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. |
يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ(11) Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, |
وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ(12) Na mkewe, na nduguye, |
وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ(13) Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, |
وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ(14) Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. |
كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ(15) La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, |
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ(16) Unao babua ngozi ya kichwa! |
تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ(17) Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. |
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ(18) Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. |
۞ إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا(19) Hakika mtu ameumbwa na papara. |
إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا(20) Inapo mgusa shari hupapatika. |
وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا(21) Na inapo mgusa kheri huizuilia. |
إِلَّا الْمُصَلِّينَ(22) Isipo kuwa wanao sali, |
الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ(23) Ambao wanadumisha Sala zao, |
وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ(24) Na ambao katika mali yao iko haki maalumu |
لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ(25) Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; |
وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ(26) Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, |
وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ(27) Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. |
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ(28) Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. |
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ(29) Na ambao wanahifadhi tupu zao. |
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ(30) Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - |
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ(31) Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. |
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ(32) Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, |
وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ(33) Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, |
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ(34) Na ambao wanazihifadhi Sala zao. |
أُولَٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ(35) Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. |
فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ(36) Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? |
عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ(37) Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! |
أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ(38) Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? |
كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ(39) La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. |
فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ(40) Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza |
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ(41) Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. |
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ(42) Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, |
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ(43) Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, |
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ(44) Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Al-Maarij : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Al-Maarij complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide