Surah Maarij aya 41 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ﴾
[ المعارج: 41]
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
Surah Al-Maarij in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
To replace them with better than them; and We are not to be outdone.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
Na kuwaleta walio watiifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao. Wala Sisi hatushindwi kubadilisha huko. Huenda ikawa inakusudiwa kwa -mashariki zote- na -magharibi zote- ni maeneo ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu yote ambayo hayana mpaka kama ilivyo ashiriwa katika Aya 137 ya Surat Al-aaraf: -Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki za nchi na magharibi zake ambayo tuliitia baraka-, kuonyesha sehemu zote za hiyo nchi inayo tajwa. Na huenda ikawa makusudio yake ni mashariki za jua na mwezi na nyota zote na sayari, na magharibi zao, kwa ajili ya kuonyesha vile vile ufalme wa Mwenyezi Mungu wote. Na kwa hivyo inadhihirika kwetu kuwa vyombo vinavyo kwenda katika qubba la mbingu vinachomoza kwenye upeo wa mashariki na kuchwa kwenye upeo wa magharibi, au kwa uchache vinazunguka kutoka mashariki kwendea magharibi kuizunguka nyota ya Pole, katika sehemu ya kaskazini ya dunia. Kwani umbali wa Pole kwa nyota ni mdogo kuliko pahala unapo angalia, basi nyota hapo haichomozi wala haichwi, bali hupiga duru ndogo kuizunguka North Pole. Na kwa hiyo Aya inaashiria saa za usiku. Rejea kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: - Na alama na kwa nyota wao wanaongoka.- Na kwa udhaahiri wa kuchomoza na kuchwa ipo ishara ya kuzunguka kwa dunia, na hiyo ni neema kubwa kabisa katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya maisha katika sayari hii. Kwani bila ya kuzunguka kwa dunia juu ya msumari-kati wake nusu ya dunia ingeli pigwa na jua mfululizo muda wa nusu mwaka kaamili, na ingeli nyimwa mwangaza kabisa nusu nyengine. Kwa hivyo uhai kama tulivyo uzoea usinge kuwako. Na tukifanya hizo mashariki na hizo magharibi ni za jua peke yake, wachilia mbali nyota nyengine na sayari, basi itakuwa ishara ni kule kuchomoza jua kila siku pahala pengine na kuchwa pahala pengine kila siku, au hata katika kila dakika linapo pita juu ya dunia. Kwani jua kila dakika linakuchwa pahala na linachomoza pahala papili mfululizo. Na haya ni katika mipango ya Mwenyezi Mungu na miujiza ya uweza wake. Tazama pia maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 5 katika Surat Assaffat, na Aya 17 ya Surat Arrahman.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza
- Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na ukiwasibu uovu kwa iliyo yatanguliza mikono yao wenyewe,
- Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini
- Wasio amini huihimiza hiyo Saa ifike upesi; lakini wanao amini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika
- Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na
- Nawapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta
- Wala hawakusema: Mungu akipenda!
- Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
- Na kwa masiku kumi,
- Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maarij with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maarij mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maarij Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



