حم(1) H'a Mim |
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ(2) Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha, |
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ(3) Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. |
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ(4) Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima, |
أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ(5) Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. |
رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ(6) Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. |
رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ(7) Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. |
لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ(8) Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. |
بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ(9) Lakini wao wanacheza katika shaka. |
فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ(10) Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, |
يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ(11) Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! |
رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ(12) Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. |
أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ(13) Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. |
ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ(14) Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. |
إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ(15) Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! |
يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ(16) Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. |
۞ وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ(17) Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. |
أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ(18) Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. |
وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ(19) Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi. |
وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ(20) Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe. |
وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ(21) Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. |
فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ(22) Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu. |
فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ(23) Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa. |
وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ(24) Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa. |
كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ(25) Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! |
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ(26) Na mimea na vyeo vitukufu! |
وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ(27) Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! |
كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ(28) Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. |
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ(29) La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula. |
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ(30) Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha, |
مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ(31) Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka. |
وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ(32) Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe. |
وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ(33) Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi. |
إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ(34) Hakika hawa wanasema: |
إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ(35) Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi. |
فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ(36) Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. |
أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ(37) Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu. |
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ(38) Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo. |
مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ(39) Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. |
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ(40) Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote. |
يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ(41) Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa. |
إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ(42) Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. |
إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ(43) Hakika Mti wa Zaqqum, |
طَعَامُ الْأَثِيمِ(44) Ni chakula cha mwenye dhambi. |
كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ(45) Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni |
كَغَلْيِ الْحَمِيمِ(46) Kama kutokota kwa maji ya moto. |
خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ(47) (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu! |
ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ(48) Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka. |
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ(49) Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! |
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ(50) Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka. |
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ(51) Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani, |
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ(52) Katika mabustani na chemchem, |
يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ(53) Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana, |
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ(54) Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini. |
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ(55) Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani. |
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ(56) Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, |
فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ(57) Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa. |
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ(58) Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka. |
فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ(59) Ngoja tu, na wao wangoje pia. |