Surah Muminun aya 20 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَشَجَرَةً تَخْرُجُ مِن طُورِ سَيْنَاءَ تَنبُتُ بِالدُّهْنِ وَصِبْغٍ لِّلْآكِلِينَ﴾
[ المؤمنون: 20]
Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.
Surah Al-Muminun in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [We brought forth] a tree issuing from Mount Sinai which produces oil and food for those who eat.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.
Na tumekuumbieni mti wa zaituni unao ota katika jimbo la Mlima wa Sinai. Katika matunda yake yanapatikana mafuta yanayo kufaeni. Na hizo zaituni ni kitoweo cha chakula kwa wanao kula. -Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.- Aya hii tukufu inathibitisha kuwa mti wa zaituni ni miongoni mwa neema alizo mneemesha Mwenyezi Mungu binaadamu na ambazo baadhi yake zimetajwa katika Aya zilizo tangulia. Na la kuongeza kwenye Aya hii ni kuwa mzaituni ni miongoni mwa miti ya mbao inayo ishi muda mrefu sana, zaidi ya mamia ya miaka. Kwa hivyo hauhitajii juhudi kubwa kwa mtu, bali huendelea kuzaa wenyewe mfululizo. Kadhaalika una sifa ya kuwa daima kijani, unapendeza kuutazama. Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha kwamba zaituni ni katika chakula kizuri. Kwani ndani yake imo Protein nyingi. Vile vile zimo chumvi za Calcium, chuma na Phospohorous. Na hivi ni muhimu na vya kutegemewa katika chakula cha binaadamu. Na juu ya hivyo zaituni inayo Vitamin A na Vitamin B. Na kutokana na tunda lake hutolewa mafuta ya zaituni, ambayo ni mafuta bora ya mafuta mepesi. Mafuta haya hutumiwa katika chakula. Uchunguzi wa kitabibu unaongeza kusema kuwa zipo faida nyengine katika mafuta ya zaituni, nazo ni kuwa zinasaidia kwa jumla katika viungo vya usagaji wa chakula, na khasa maini. Nayo yanashinda ubora mafuta yote yanayo tokana na mimea na wanyama, kwa kuwa hayasabibishi maradhi ya mishipa ya damu kama mafuta mengineyo, na kadhaalika yanalainisha ngozi. Na mafuta ya zaituni yana matumizi mengine mengi katika sanaa (ufundi), kwani yanatumiwa katika kufanya sabuni nzuri kabisa, na vitu vinginevyo katika ufanyaji wa vyakula na vitu vya sanaa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa
- Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.
- Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo
- Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?
- Au mnadhani mko salama kwa alioko juu ya kuwa Yeye hakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Mtajua
- Na zinazo kwenda kwa wepesi.
- Na Musa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote waliomo duniani, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, Anajitosha,
- Na hao mnao waomba asiye kuwa Mwenyezi hawawezi kukunusuruni, wala hawajinusuru wenyewe.
- Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na
- Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Muminun with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Muminun mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Muminun Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers