Surah Furqan aya 45 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ الظِّلَّ وَلَوْ شَاءَ لَجَعَلَهُ سَاكِنًا ثُمَّ جَعَلْنَا الشَّمْسَ عَلَيْهِ دَلِيلًا﴾
[ الفرقان: 45]
Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na angeli taka angeli kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
Surah Al-Furqan in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Have you not considered your Lord - how He extends the shadow, and if He willed, He could have made it stationary? Then We made the sun for it an indication.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na angeli taka angeli kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
Tumesimamisha dalili za Tawhidi, Upweke wa Mwenyezi Mungu, za kuwaongoa wenye akili. Hebu kiangalie kivuli. Mwenyezi Mungu amekitandaza na akakifanya kimetulia mwanzo wa mchana. Kisha tukalipeleka jua likaondoa pahala pake kwa mwako wake. Likawa jua ni kama ndio linaongoza kivuli. Bila ya jua, kivuli kisingeli juulikana. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda angeli kifanya kivuli kitulie vile vile kimewangangania watu, na yakawaharibikia maslaha yao na mambo yao. - Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na angeli taka angeli kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.- Aya hii inadhihirisha hima ya Muumba na uwezo wake. Kwani kutandaza kivuli kunaonyesha mzunguko wa dunia na kuinama kwa msumari-kati (axis) wake. Na lau kuwa ardhi, yaani dunia, ingeli tulia tu, haitaharaki kulizunguka jua, na pia ikawa haizunguki wenyewe kwa wenyewe juu ya msumari-kati wake, basi kivuli kingeli tulia, na mwako wa jua ungeli piga juu ya nusu ya dunia, na nusu ya pili ikabaki ni usiku, moja kwa moja. Hayo yangeli leta khitilafu kubwa za baridi na joto, na ingeli pelekea kutoweka uhai kabisa katika dunia. Na kadhaalika ingeli kuwa hii ni hali ya dunia basi kivuli kingeli tulia. Na haya pia yange tokea ikiwa muda wa kuzunguka ardhi juu ya msumari-kati wake ndio muda ule ule muda wa kuzunguka kwake kulizunguka jua, yaani siku moja ikawa sawa na mwaka mzima. Lakini hapana awezaye kufanya hayo isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Haya licha ya kuwa kivuli nafsi yake ni neema miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu aliviumba vitu vyote vyapenyeza mwangaza (transparent) kisingeli kuwapo kivuli, na vitu visingeli pata fursa ya kuwepo ambavyo vinahitajia vivuli.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
- Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu kali.
- Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni
- Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
- Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na
- Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo kuwa
- Sema: Ingeli kuwa duniani wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya shaka tungeli
- Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
- Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako
- Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Furqan with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Furqan mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Furqan Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers