La sourate Al-Waqiah en Swahili
إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ(1) Litakapo tukia hilo Tukio |
لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ(2) Hapana cha kukanusha kutukia kwake. |
خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ(3) Literemshalo linyanyualo, |
إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا(4) Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso, |
وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا(5) Na milima itapo sagwasagwa, |
فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا(6) Iwe mavumbi yanayo peperushwa, |
وَكُنتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً(7) Na nyinyi mtakuwa namna tatu:- |
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ(8) Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? |
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ(9) Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? |
وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ(10) Na wa mbele watakuwa mbele. |
أُولَٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ(11) Hao ndio watakao karibishwa |
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ(12) Katika Bustani zenye neema. |
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ(13) Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ(14) Na wachache katika wa mwisho. |
عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ(15) Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. |
مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ(16) Wakiviegemea wakielekeana. |
يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ(17) Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, |
بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ(18) Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. |
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ(19) Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. |
وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ(20) Na matunda wayapendayo, |
وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ(21) Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. |
وَحُورٌ عِينٌ(22) Na Mahurulaini, |
كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ(23) Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. |
جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ(24) Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. |
لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا(25) Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, |
إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا(26) Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. |
وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ(27) Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? |
فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ(28) Katika mikunazi isiyo na miba, |
وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ(29) Na migomba iliyo pangiliwa, |
وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ(30) Na kivuli kilicho tanda, |
وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ(31) Na maji yanayo miminika, |
وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ(32) Na matunda mengi, |
لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ(33) Hayatindikii wala hayakatazwi, |
وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ(34) Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. |
إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً(35) Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, |
فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا(36) Na tutawafanya vijana, |
عُرُبًا أَتْرَابًا(37) Wanapendana na waume zao, hirimu moja. |
لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ(38) Kwa ajili ya watu wa kuliani. |
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ(39) Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ(40) Na fungu kubwa katika wa mwisho. |
وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ(41) Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? |
فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ(42) Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, |
وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ(43) Na kivuli cha moshi mweusi, |
لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ(44) Si cha kuburudisha wala kustarehesha. |
إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ(45) Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. |
وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ(46) Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, |
وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ(47) Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? |
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ(48) Au baba zetu wa zamani? |
قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ(49) Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho |
لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ(50) Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. |
ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ(51) Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, |
لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ(52) Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. |
فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ(53) Na kwa mti huo mtajaza matumbo. |
فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ(54) Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. |
فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ(55) Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. |
هَٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ(56) Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. |
نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ(57) Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? |
أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ(58) Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? |
أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ(59) Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? |
نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ(60) Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi |
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ(61) Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. |
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ(62) Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? |
أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ(63) Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? |
أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ(64) Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? |
لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ(65) Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, |
إِنَّا لَمُغْرَمُونَ(66) Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; |
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ(67) Bali sisi tumenyimwa. |
أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ(68) Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? |
أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ(69) Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? |
لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ(70) Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? |
أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ(71) Je! Mnauona moto mnao uwasha? |
أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ(72) Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? |
نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِّلْمُقْوِينَ(73) Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. |
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ(74) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. |
۞ فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ(75) Basi naapa kwa maanguko ya nyota, |
وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ(76) Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! |
إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ(77) Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, |
فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ(78) Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. |
لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ(79) Hapana akigusaye ila walio takaswa. |
تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ(80) Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
أَفَبِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ(81) Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? |
وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ(82) Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? |
فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ(83) Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, |
وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ(84) Na nyinyi wakati huo mnatazama! |
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ(85) Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. |
فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ(86) Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, |
تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ(87) Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? |
فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ(88) Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, |
فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ(89) Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. |
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ(90) Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, |
فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ(91) Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. |
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ(92) Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, |
فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ(93) Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, |
وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ(94) Na kutiwa Motoni. |
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ(95) Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. |
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ(96) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Al-Waqiah : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Al-Waqiah complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide