8 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮣﮤﮥ
102:1 Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
ﮦﮧﮨﮩ
102:2 Mpaka mje makaburini!
ﮪﮫﮬﮭ
102:3 Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
ﮮﮯﮰﮱﯓ
102:4 Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
ﯔﯕﯖﯗﯘﯙ
102:5 Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
ﯚﯛﯜ
102:6 Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
ﯝﯞﯟﯠﯡ
102:7 Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
ﯢﯣﯤﯥﯦﯧ
102:8 Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.

Kurani Tukufu


Tuesday, September 29, 2026

Usitusahau katika dua zako njema