PDF —
25 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Inshiqaq pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Inshiqaq pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Inshiqaq Tafsiri. Sura Al-Inshiqaq (Makka) 25 Aya.



25 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﭣﭤﭥﭦ
84:1 Itapo chanika mbingu,
ﭧﭨﭩﭪ
84:2 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
ﭫﭬﭭﭮ
84:3 Na ardhi itakapo tanuliwa,
ﭯﭰﭱﭲﭳ
84:4 Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
ﭴﭵﭶﭷ
84:5 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
ﭸﭹﭺﭻﭼﭽﭾﭿﮀ
84:6 Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
ﮁﮂﮃﮄﮅﮆ
84:7 Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
ﮇﮈﮉﮊﮋ
84:8 Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
ﮌﮍﮎﮏﮐ
84:9 Na arudi kwa ahali zake na furaha.
ﮑﮒﮓﮔﮕﮖﮗ
84:10 Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
ﮘﮙﮚﮛ
84:11 Basi huyo ataomba kuteketea.
ﮜﮝﮞ
84:12 Na ataingia Motoni.
ﮟﮠﮡﮢﮣﮤ
84:13 Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
ﮥﮦﮧﮨﮩﮪ
84:14 Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
ﮫﮬﮭﮮﮯﮰﮱﯓ
84:15 Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
ﯔﯕﯖﯗ
84:16 Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
ﯘﯙﯚﯛ
84:17 Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
ﯜﯝﯞﯟ
84:18 Na kwa mwezi unapo pevuka,
ﯠﯡﯢﯣﯤ
84:19 Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
ﯥﯦﯧﯨﯩ
84:20 Basi wana nini hawaamini?
ﯪﯫﯬﯭﯮﯯﯰﯱ
84:21 Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
ﯲﯳﯴﯵﯶ
84:22 Bali walio kufuru wanakanusha tu.
ﯷﯸﯹﯺﯻ
84:23 Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
ﯼﯽﯾﯿ
84:24 Basi wabashirie adhabu chungu!
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗﭘﭙﭚ
84:25 Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema