Sura Al-Ghashiya pdf — Pakua (Kiswahili)
Sura Al-Ghashiya pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Ghashiya Tafsiri. Sura Al-Ghashiya (Makka) 26 Aya.
Related
- Sura Al-Ghashiya TafsiriKiswahili
- Sura Al-Ghashiya mp3Sikiliza
- Quran Index Kiswahili114
More Sura PDF
Sura Al-Ghashiya

ﭽﭾﭿﮀﮁ
88:1
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
ﮂﮃﮄﮅ
88:2
Siku hiyo nyuso zitainama,
ﮆﮇﮈ
88:3
Zikifanya kazi, nazo taabani.
ﮉﮊﮋﮌ
88:4
Ziingie katika Moto unao waka -
ﮍﮎﮏﮐﮑ
88:5
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
ﮒﮓﮔﮕﮖﮗﮘ
88:6
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
ﮙﮚﮛﮜﮝﮞﮟ
88:7
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
ﮠﮡﮢﮣ
88:8
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
ﮤﮥﮦ
88:9
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
ﮧﮨﮩﮪ
88:10
Katika Bustani ya juu.
ﮫﮬﮭﮮﮯ
88:11
Hawatasikia humo upuuzi.
ﮰﮱﯓﯔ
88:12
Humo imo chemchem inayo miminika.
ﯕﯖﯗﯘ
88:13
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
ﯙﯚﯛ
88:14
Na bilauri zilizo pangwa,
ﯜﯝﯞ
88:15
Na matakia safu safu,
ﯟﯠﯡ
88:16
Na mazulia yaliyo tandikwa.
ﯢﯣﯤﯥﯦﯧﯨ
88:17
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
ﯩﯪﯫﯬﯭ
88:18
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
ﯮﯯﯰﯱﯲ
88:19
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
ﯳﯴﯵﯶﯷ
88:20
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
ﯸﯹﯺﯻﯼ
88:21
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
ﯽﯾﯿﰀ
88:22
Wewe si mwenye kuwatawalia.
ﭑﭒﭓﭔﭕ
88:23
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
ﭖﭗﭘﭙﭚ
88:24
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
ﭛﭜﭝﭞ
88:25
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
ﭟﭠﭡﭢﭣ
88:26
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
Kurani Tukufu
Wednesday, September 9, 2026
Usitusahau katika dua zako njema







