PDF —
96 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Waqi'a pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Waqi'a pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Waqi'a Tafsiri. Sura Al-Waqi'a (Makka) 96 Aya.



96 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮃﮄﮅﮆ
56:1 Litakapo tukia hilo Tukio
ﮇﮈﮉﮊ
56:2 Hapana cha kukanusha kutukia kwake.
ﮋﮌﮍ
56:3 Literemshalo linyanyualo,
ﮎﮏﮐﮑﮒ
56:4 Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso,
ﮓﮔﮕﮖ
56:5 Na milima itapo sagwasagwa,
ﮗﮘﮙﮚ
56:6 Iwe mavumbi yanayo peperushwa,
ﮛﮜﮝﮞ
56:7 Na nyinyi mtakuwa namna tatu:-
ﮟﮠﮡﮢﮣﮤ
56:8 Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
ﮥﮦﮧﮨﮩﮪ
56:9 Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
ﮫﮬﮭ
56:10 Na wa mbele watakuwa mbele.
ﮮﮯﮰ
56:11 Hao ndio watakao karibishwa
ﮱﯓﯔﯕ
56:12 Katika Bustani zenye neema.
ﯖﯗﯘﯙ
56:13 Fungu kubwa katika wa mwanzo,
ﯚﯛﯜﯝ
56:14 Na wachache katika wa mwisho.
ﯞﯟﯠﯡ
56:15 Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
ﯢﯣﯤﯥ
56:16 Wakiviegemea wakielekeana.
ﭑﭒﭓﭔﭕ
56:17 Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
ﭖﭗﭘﭙﭚﭛ
56:18 Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
ﭜﭝﭞﭟﭠﭡ
56:19 Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
ﭢﭣﭤﭥ
56:20 Na matunda wayapendayo,
ﭦﭧﭨﭩﭪ
56:21 Na nyama za ndege kama wanavyo tamani.
ﭫﭬﭭ
56:22 Na Mahurulaini,
ﭮﭯﭰﭱ
56:23 Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
ﭲﭳﭴﭵﭶ
56:24 Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
ﭷﭸﭹﭺﭻﭼﭽ
56:25 Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
ﭾﭿﮀﮁﮂ
56:26 Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
ﮃﮄﮅﮆﮇﮈ
56:27 Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?
ﮉﮊﮋﮌ
56:28 Katika mikunazi isiyo na miba,
ﮍﮎﮏ
56:29 Na migomba iliyo pangiliwa,
ﮐﮑﮒ
56:30 Na kivuli kilicho tanda,
ﮓﮔﮕ
56:31 Na maji yanayo miminika,
ﮖﮗﮘ
56:32 Na matunda mengi,
ﮙﮚﮛﮜﮝ
56:33 Hayatindikii wala hayakatazwi,
ﮞﮟﮠ
56:34 Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.
ﮡﮢﮣﮤ
56:35 Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
ﮥﮦﮧ
56:36 Na tutawafanya vijana,
ﮨﮩﮪ
56:37 Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
ﮫﮬﮭ
56:38 Kwa ajili ya watu wa kuliani.
ﮮﮯﮰﮱ
56:39 Fungu kubwa katika wa mwanzo,
ﯓﯔﯕﯖ
56:40 Na fungu kubwa katika wa mwisho.
ﯗﯘﯙﯚﯛﯜ
56:41 Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
ﯝﯞﯟﯠ
56:42 Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
ﯡﯢﯣﯤ
56:43 Na kivuli cha moshi mweusi,
ﯥﯦﯧﯨﯩ
56:44 Si cha kuburudisha wala kustarehesha.
ﯪﯫﯬﯭﯮﯯ
56:45 Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.
ﯰﯱﯲﯳﯴﯵ
56:46 Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,
ﯶﯷﯸﯹﯺﯻﯼﯽﯾﯿ
56:47 Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
ﰀﰁﰂ
56:48 Au baba zetu wa zamani?
ﰃﰄﰅﰆﰇ
56:49 Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
ﰈﰉﰊﰋﰌﰍ
56:50 Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖ
56:51 Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
ﭗﭘﭙﭚﭛﭜ
56:52 Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
ﭝﭞﭟﭠ
56:53 Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
ﭡﭢﭣﭤﭥ
56:54 Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
ﭦﭧﭨﭩ
56:55 Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.
ﭪﭫﭬﭭﭮ
56:56 Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
ﭯﭰﭱﭲﭳ
56:57 Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
ﭴﭵﭶﭷ
56:58 Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
ﭸﭹﭺﭻﭼﭽ
56:59 Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
ﭾﭿﮀﮁﮂﮃﮄﮅ
56:60 Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
ﮆﮇﮈﮉﮊﮋﮌﮍﮎﮏ
56:61 Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
ﮐﮑﮒﮓﮔﮕﮖ
56:62 Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
ﮗﮘﮙﮚ
56:63 Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?
ﮛﮜﮝﮞﮟﮠ
56:64 Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
ﮡﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
56:65 Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu,
ﮨﮩﮪ
56:66 Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;
ﮫﮬﮭﮮ
56:67 Bali sisi tumenyimwa.
ﮯﮰﮱﯓﯔ
56:68 Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?
ﯕﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜ
56:69 Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
ﯝﯞﯟﯠﯡﯢﯣ
56:70 Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
ﯤﯥﯦﯧﯨ
56:71 Je! Mnauona moto mnao uwasha?
ﯩﯪﯫﯬﯭﯮﯯ
56:72 Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
ﯰﯱﯲﯳﯴﯵ
56:73 Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.
ﯶﯷﯸﯹﯺ
56:74 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
ﯻﯼﯽﯾﯿﰀ
56:75 Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
ﰁﰂﰃﰄﰅﰆ
56:76 Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
ﭑﭒﭓﭔ
56:77 Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
ﭕﭖﭗﭘ
56:78 Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.
ﭙﭚﭛﭜﭝ
56:79 Hapana akigusaye ila walio takaswa.
ﭞﭟﭠﭡﭢ
56:80 Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
ﭣﭤﭥﭦﭧ
56:81 Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
ﭨﭩﭪﭫﭬ
56:82 Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
ﭭﭮﭯﭰﭱ
56:83 Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
ﭲﭳﭴﭵ
56:84 Na nyinyi wakati huo mnatazama!
ﭶﭷﭸﭹﭺﭻﭼﭽ
56:85 Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
ﭾﭿﮀﮁﮂﮃ
56:86 Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
ﮄﮅﮆﮇﮈ
56:87 Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
ﮉﮊﮋﮌﮍﮎ
56:88 Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
ﮏﮐﮑﮒﮓ
56:89 Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
ﮔﮕﮖﮗﮘﮙﮚ
56:90 Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,
ﮛﮜﮝﮞﮟﮠ
56:91 Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.
ﮡﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
56:92 Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
ﮨﮩﮪﮫ
56:93 Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,
ﮬﮭﮮ
56:94 Na kutiwa Motoni.
ﮯﮰﮱﯓﯔﯕ
56:95 Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
ﯖﯗﯘﯙﯚ
56:96 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema