Sura Al-A'la pdf — Pakua (Kiswahili)
Sura Al-A'la pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-A'la Tafsiri. Sura Al-A'la (Makka) 19 Aya.
Related
- Sura Al-A'la TafsiriKiswahili
- Sura Al-A'la mp3Sikiliza
- Quran Index Kiswahili114
More Sura PDF
Sura Al-A'la

ﮟﮠﮡﮢﮣ
87:1
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
ﮤﮥﮦﮧ
87:2
Aliye umba, na akaweka sawa,
ﮨﮩﮪﮫ
87:3
Na ambaye amekadiria na akaongoa,
ﮬﮭﮮﮯ
87:4
Na aliye otesha malisho,
ﮰﮱﯓﯔ
87:5
Kisha akayafanya makavu, meusi.
ﯕﯖﯗﯘ
87:6
Tutakusomesha wala hutasahau,
ﯙﯚﯛﯜﯝﯞﯟﯠﯡﯢﯣ
87:7
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
ﯤﯥﯦ
87:8
Na tutakusahilishia yawe mepesi.
ﯧﯨﯩﯪﯫ
87:9
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
ﯬﯭﯮﯯ
87:10
Atakumbuka mwenye kuogopa.
ﭑﭒﭓ
87:11
Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
ﭔﭕﭖﭗﭘ
87:12
Ambaye atauingia Moto mkubwa.
ﭙﭚﭛﭜﭝﭞﭟ
87:13
Tena humo hatakufa wala hawi hai.
ﭠﭡﭢﭣﭤ
87:14
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
ﭥﭦﭧﭨﭩ
87:15
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
ﭪﭫﭬﭭﭮ
87:16
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
ﭯﭰﭱﭲ
87:17
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
ﭳﭴﭵﭶﭷﭸ
87:18
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
ﭹﭺﭻﭼ
87:19
Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
Kurani Tukufu
Wednesday, September 9, 2026
Usitusahau katika dua zako njema







