PDF —
52 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Haqqa pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Haqqa pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Haqqa Tafsiri. Sura Al-Haqqa (Makka) 52 Aya.



52 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮯﮰ
69:1 Tukio la haki.
ﮱﯓﯔ
69:2 Nini hilo Tukio la haki?
ﯕﯖﯗﯘﯙ
69:3 Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?
ﯚﯛﯜﯝﯞ
69:4 Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
ﯟﯠﯡﯢﯣ
69:5 Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
ﯤﯥﯦﯧﯨﯩﯪ
69:6 Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
ﯫﯬﯭﯮﯯﯰﯱﯲﯳﯴﯵﯶﯷﯸﯹﯺﯻ
69:7 Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
ﯼﯽﯾﯿﰀﰁ
69:8 Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗ
69:9 Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.
ﭘﭙﭚﭛﭜﭝﭞ
69:10 Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
ﭟﭠﭡﭢﭣﭤﭥﭦ
69:11 Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,
ﭧﭨﭩﭪﭫﭬﭭ
69:12 Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.
ﭮﭯﭰﭱﭲﭳﭴ
69:13 Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,
ﭵﭶﭷﭸﭹﭺﭻ
69:14 Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,
ﭼﭽﭾﭿ
69:15 Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
ﮀﮁﮂﮃﮄﮅ
69:16 Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
ﮆﮇﮈﮉﮊﮋﮌﮍﮎﮏﮐ
69:17 Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
ﮑﮒﮓﮔﮕﮖﮗ
69:18 Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
ﮘﮙﮚﮛﮜﮝﮞﮟﮠﮡ
69:19 Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
ﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
69:20 Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
ﮨﮩﮪﮫﮬ
69:21 Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,
ﮭﮮﮯﮰ
69:22 Katika Bustani ya juu,
ﮱﯓﯔ
69:23 Matunda yake yakaribu.
ﯕﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜﯝ
69:24 Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣﯤﯥﯦﯧﯨ
69:25 Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!
ﯩﯪﯫﯬﯭ
69:26 Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.
ﯮﯯﯰﯱ
69:27 Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
ﯲﯳﯴﯵﯶﯷ
69:28 Mali yangu hayakunifaa kitu.
ﯸﯹﯺﯻ
69:29 Madaraka yangu yamenipotea.
ﯼﯽﯾ
69:30 (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
ﯿﰀﰁﰂ
69:31 Kisha mtupeni Motoni!
ﰃﰄﰅﰆﰇﰈﰉﰊ
69:32 Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!
ﰋﰌﰍﰎﰏﰐﰑ
69:33 Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,
ﰒﰓﰔﰕﰖﰗ
69:34 Wala hahimizi kulisha masikini.
ﰘﰙﰚﰛﰜﰝ
69:35 Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖ
69:36 Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
ﭗﭘﭙﭚﭛ
69:37 Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
ﭜﭝﭞﭟﭠ
69:38 Basi naapa kwa mnavyo viona,
ﭡﭢﭣﭤ
69:39 Na msivyo viona,
ﭥﭦﭧﭨﭩ
69:40 Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
ﭪﭫﭬﭭﭮﭯﭰﭱﭲ
69:41 Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
ﭳﭴﭵﭶﭷﭸﭹﭺ
69:42 Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
ﭻﭼﭽﭾﭿ
69:43 Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
ﮀﮁﮂﮃﮄﮅ
69:44 Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
ﮆﮇﮈﮉ
69:45 Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
ﮊﮋﮌﮍﮎ
69:46 Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
ﮏﮐﮑﮒﮓﮔﮕ
69:47 Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
ﮖﮗﮘﮙ
69:48 Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
ﮚﮛﮜﮝﮞﮟ
69:49 Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
ﮠﮡﮢﮣﮤ
69:50 Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
ﮥﮦﮧﮨ
69:51 Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
ﮩﮪﮫﮬﮭ
69:52 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema