5 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮈﮉﮊﮋﮌﮍ
111:1 Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
ﮎﮏﮐﮑﮒﮓﮔ
111:2 Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
ﮕﮖﮗﮘﮙ
111:3 Atauingia Moto wenye mwako.
ﮚﮛﮜﮝ
111:4 Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
ﮞﮟﮠﮡﮢﮣ
111:5 Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.

Kurani Tukufu


Tuesday, September 29, 2026

Usitusahau katika dua zako njema