8 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﯝﯞﯟﯠﯡ
94:1 Hatukukunjulia kifua chako?
ﯢﯣﯤﯥ
94:2 Na tukakuondolea mzigo wako,
ﭑﭒﭓﭔ
94:3 Ulio vunja mgongo wako?
ﭕﭖﭗﭘ
94:4 Na tukakunyanyulia utajo wako?
ﭙﭚﭛﭜﭝ
94:5 Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
ﭞﭟﭠﭡﭢ
94:6 Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
ﭣﭤﭥﭦ
94:7 Na ukipata faragha, fanya juhudi.
ﭧﭨﭩﭪ
94:8 Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.

Kurani Tukufu


Tuesday, September 29, 2026

Usitusahau katika dua zako njema