11 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮉﮊ
93:1 Naapa kwa mchana!
ﮋﮌﮍﮎ
93:2 Na kwa usiku unapo tanda!
ﮏﮐﮑﮒﮓﮔ
93:3 Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
ﮕﮖﮗﮘﮙﮚ
93:4 Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
ﮛﮜﮝﮞﮟ
93:5 Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
ﮠﮡﮢﮣﮤ
93:6 Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
ﮥﮦﮧﮨ
93:7 Na akakukuta umepotea akakuongoa?
ﮩﮪﮫﮬ
93:8 Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
ﮭﮮﮯﮰﮱ
93:9 Basi yatima usimwonee!
ﯓﯔﯕﯖﯗ
93:10 Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
ﯘﯙﯚﯛﯜ
93:11 Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.

Kurani Tukufu


Tuesday, September 29, 2026

Usitusahau katika dua zako njema