Mishary Rashid Alafasy
✓
Mahmoud Khalil Al-Husary
✓
Abdurrahman As-Sudais
✓
Mohamed Siddiq Al-Minshawi
✓
Abdul Basit Abdul Samad
✓
Ali Al-Hudhaify
✓
Ahmed ibn Ali al-Ajamy
✓
Abu Bakr Ash-Shaatree
✓
Muhammad Ayyoub
✓
Abdullah Basfar
✓
Abdullah Al-Juhani
✓
Maher Al Muaiqly
✓
Tafsiri — Tafsir
Maana ya Maneno:
- Zumaran: Makundi kwa makundi, wakiwa wamepangwa kwa utaratibu na heshima.
- Khazanatuha: Malaika walio wakezwa kwa ajili ya kuhifadhi na kusimamia milango ya Pepo.
- Tibtum: Mlio kuwa wema na safi; wamekuwa wenye hali njema katika imani na matendo yenu.
Ufafanuzi wa Aya:
Mwenyezi Mungu anaelezea hali ya waumini wanaomcha Mola wao, ambao walimtii kwa kufuata amri zake na kujiepusha na makatazo yake. Malaika watawasindikiza kwa upole na heshima hadi Peponi, wakiwa katika makundi makundi yaliyopangwa kwa utaratibu mzuri, tofauti na wakosefu watakao fukuzwa Motoni kwa fedheha. Wanapofika kwenye milango ya Pepo, milango hiyo itafunguliwa kwa ajili yao kama ishara ya kukaribishwa, na Malaika walio wakezwa kwa Pepo watawatangazia salamu za amani na furaha, wakiwaambia: "Amani iwe juu yenu, mmeondokana na kila baya na kila kitu mnachokichukia. Mme kuwa wema na safi katika imani na matendo yenu, basi ingieni Peponi mkidumu humo milele, bila ya kufa wala kutolewa." Hii ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake wema, ambapo hukaribishwa kwa furaha kubwa na heshima ya kipekee.
Faida Zinazotokana na Aya:
- Fadhila ya kumcha Mwenyezi Mungu: Aya hii inaonyesha kwamba kumcha Mungu kwa kufuata amri zake na kujiepusha na makatazo yake ndio njia ya kufikia Pepo, na kwamba Mwenyezi Mungu huwapa waumini wake heshima kubwa Siku ya Kiyama.
- Heshima ya Malaika kwa waumini: Malaika watawakaribisha waumini kwa maneno ya salamu na furaha, jambo linaloonyesha hadhi kubwa ya waumini mbele ya Mwenyezi Mungu na viumbe wake.
- Kutakasika kwa waumini: Maneno "Tibtum" yanaashiria kwamba waumini wataingia Peponi wakiwa safi kutokana na dhambi na makosa, kwani Mwenyezi Mungu huwatakasa na kuwafuta dhambi zao.
- Kudumu katika Pepo: Aya inathibitisha kwamba waumini wataishi Peponi milele bila ya kufa, jambo linalowapa matumaini makubwa na kuwatia moyo kusubiri kwa subira na kujitahidi katika ibada.
- Kutia hamu ya kufanya mema: Kujua kwamba mwisho wa wachamungu ni furaha na heshima hii kubwa humfanya Muumini ajitahidi zaidi katika matendo mema na kuepuka maovu, kwa kuwa anajua kwamba matokeo ya kumcha Mungu ni ya kudumu na ya furaha isiyo na mwisho.
📜 Aya 71-75 — Sura Az-Zumar
Tafsiri — Az-Zumar 73
Sura Az-Zumar Aya 73 - Soma, Sikiliza, Tafsiri, Kiswahili : Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa…Sura Aya 73/75 — Sura Az-Zumar الزمر (Makka). Soma Sikiliza Tafsiri (Kiswahili). Sikiliza: Sura Az-Zumar Sikiliza, Sura Az-Zumar Tafsiri, Sura Az-Zumar mp3, Sura Az-Zumar pdf. Aya 71–75. Kwa Kiswahili: Soomaali.
Kurani Tukufu
Thursday, October 1, 2026
Usitusahau katika dua zako njema


