At-Tawba · 16/129
Tafsiri Uandishi wa sauti — At-Tawba
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ۝١٦
Am hasibtum an turakoo wa lammaa ya`lamil laahul lazeena jaahadoo minkum wa lam yattakhizoo min doonil laahi wa laa Rasoolihee wa lalmu`mineena waleejah; wallaahu khabeerum bimaa ta`maloon
📖 Kwa Kiswahili
Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, bila ya Mwenyezi Mungu kuwajuulisha wale walio pigana Jihadi kati yenu, na wala hawakumfanya mwendani wao isipo kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
🎧 Sikiliza

📜 Aya 14-18 — At-Tawba

14قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ
Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini,
15وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ اللَّهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba ya amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.
16أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ
Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, bila ya Mwenyezi Mungu kuwajuulisha wale walio pigana Jihadi kati yenu, na wala hawakumfanya mwendani wao isipo kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
17مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنفُسِهِم بِالْكُفْرِ ۚ أُولَٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ
Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika, na katika Moto watadumu.
18إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ
Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.
At-TawbaFaharasa ya Qurani
129Aya
MadinaRevelation
16Aya

Tafsiri — At-Tawba 16

Sura At-Tawba Aya 16 - Soma, Sikiliza, Tafsiri, Kiswahili : Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, bila ya Mwenyezi Mungu kuwajuulisha…

Sura Aya 16/129 — At-Tawba التوبة (Madina). Soma Sikiliza Tafsiri (Kiswahili). Sikiliza: At-Tawba Sikiliza, At-Tawba Tafsiri, At-Tawba mp3, At-Tawba pdf. Aya 14–18. Kwa Kiswahili: Soomaali.




Kurani Tukufu


Tuesday, August 18, 2026

Usitusahau katika dua zako njema