Sura Al-'Adiyat pdf — Pakua (Kiswahili)
Sura Al-'Adiyat pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-'Adiyat Tafsiri. Sura Al-'Adiyat (Makka) 11 Aya.
Related
- Sura Al-'Adiyat TafsiriKiswahili
- Sura Al-'Adiyat mp3Sikiliza
- Quran Index Kiswahili114
More Sura PDF
Sura Al-'Adiyat

ﮱﯓﯔ
100:1
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
ﯕﯖﯗ
100:2
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
ﯘﯙﯚ
100:3
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
ﯛﯜﯝﯞ
100:4
Huku wakitimua vumbi,
ﯟﯠﯡﯢ
100:5
Na wakijitoma kati ya kundi,
ﭑﭒﭓﭔﭕ
100:6
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
ﭖﭗﭘﭙﭚ
100:7
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
ﭛﭜﭝﭞﭟ
100:8
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
ﭠﭡﭢﭣﭤﭥﭦﭧﭨ
100:9
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
ﭩﭪﭫﭬﭭ
100:10
Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
ﭮﭯﭰﭱﭲﭳ
100:11
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
Kurani Tukufu
Wednesday, September 9, 2026
Usitusahau katika dua zako njema







