PDF —
21 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Layl pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Layl pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Layl Tafsiri. Sura Al-Layl (Makka) 21 Aya.



21 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮡﮢﮣﮤ
92:1 Naapa kwa usiku unapo funika!
ﮥﮦﮧﮨ
92:2 Na mchana unapo dhihiri!
ﮩﮪﮫﮬﮭ
92:3 Na kwa Aliye umba dume na jike!
ﮮﮯﮰﮱ
92:4 Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
ﯓﯔﯕﯖﯗ
92:5 Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
ﯘﯙﯚ
92:6 Na akaliwafiki lilio jema,
ﯛﯜﯝ
92:7 Tutamsahilishia yawe mepesi.
ﯞﯟﯠﯡﯢ
92:8 Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
ﯣﯤﯥ
92:9 Na akakanusha lilio jema,
ﭑﭒﭓ
92:10 Tutamsahilishia yawe mazito!
ﭔﭕﭖﭗﭘﭙﭚ
92:11 Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
ﭛﭜﭝﭞ
92:12 Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
ﭟﭠﭡﭢﭣ
92:13 Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
ﭤﭥﭦﭧ
92:14 Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
ﭨﭩﭪﭫﭬ
92:15 Hatauingia ila mwovu kabisa!
ﭭﭮﭯﭰ
92:16 Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
ﭱﭲﭳ
92:17 Na mchamngu ataepushwa nao,
ﭴﭵﭶﭷﭸ
92:18 Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
ﭹﭺﭻﭼﭽﭾﭿ
92:19 Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
ﮀﮁﮂﮃﮄﮅ
92:20 Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
ﮆﮇﮈ
92:21 Naye atakuja ridhika!

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema