PDF —
44 Aya Makka PDF
Built right in your browser — download starts automatically

Sura Al-Ma'arij pdf — Pakua (Kiswahili)

Sura Al-Ma'arij pdf Kiswahili — Pakua Sura Al-Ma'arij Tafsiri. Sura Al-Ma'arij (Makka) 44 Aya.

← Al-HaqqaSura Al-Ma'arij Nuh →


44 Aya · Makka · Kiswahili
bismillah
ﮮﮯﮰﮱﯓ
70:1 Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea,
ﯔﯕﯖﯗﯘ
70:2 Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia -
ﯙﯚﯛﯜﯝ
70:3 Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
ﯞﯟﯠﯡﯢﯣﯤﯥﯦﯧﯨﯩ
70:4 Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!
ﯪﯫﯬﯭ
70:5 Basi subiri kwa subira njema.
ﯮﯯﯰﯱ
70:6 Hakika wao wanaiona iko mbali,
ﯲﯳﯴ
70:7 Na Sisi tunaiona iko karibu.
ﯵﯶﯷﯸﯹ
70:8 Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa.
ﯺﯻﯼﯽ
70:9 Na milima itakuwa kama sufi.
ﯾﯿﰀﰁﰂ
70:10 Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗﭘﭙﭚﭛ
70:11 Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe,
ﭜﭝﭞ
70:12 Na mkewe, na nduguye,
ﭟﭠﭡﭢ
70:13 Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu,
ﭣﭤﭥﭦﭧﭨﭩ
70:14 Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
ﭪﭫﭬﭭﭮ
70:15 La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,
ﭯﭰﭱ
70:16 Unao babua ngozi ya kichwa!
ﭲﭳﭴﭵﭶ
70:17 Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.
ﭷﭸﭹ
70:18 Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.
ﭺﭻﭼﭽﭾﭿ
70:19 Hakika mtu ameumbwa na papara.
ﮀﮁﮂﮃﮄ
70:20 Inapo mgusa shari hupapatika.
ﮅﮆﮇﮈﮉ
70:21 Na inapo mgusa kheri huizuilia.
ﮊﮋﮌ
70:22 Isipo kuwa wanao sali,
ﮍﮎﮏﮐﮑﮒ
70:23 Ambao wanadumisha Sala zao,
ﮓﮔﮕﮖﮗﮘ
70:24 Na ambao katika mali yao iko haki maalumu
ﮙﮚﮛ
70:25 Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba;
ﮜﮝﮞﮟﮠ
70:26 Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,
ﮡﮢﮣﮤﮥﮦﮧ
70:27 Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.
ﮨﮩﮪﮫﮬﮭ
70:28 Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.
ﮮﮯﮰﮱﯓ
70:29 Na ambao wanahifadhi tupu zao.
ﯔﯕﯖﯗﯘﯙﯚﯛﯜﯝﯞ
70:30 Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi -
ﯟﯠﯡﯢﯣﯤﯥﯦ
70:31 Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
ﯧﯨﯩﯪﯫﯬ
70:32 Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,
ﯭﯮﯯﯰﯱ
70:33 Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,
ﯲﯳﯴﯵﯶﯷ
70:34 Na ambao wanazihifadhi Sala zao.
ﯸﯹﯺﯻﯼ
70:35 Hao ndio watakao hishimiwa Peponi.
ﯽﯾﯿﰀﰁﰂ
70:36 Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu?
ﰃﰄﰅﰆﰇﰈ
70:37 Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!
ﰉﰊﰋﰌﰍﰎﰏﰐﰑ
70:38 Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?
ﰒﰓﰔﰕﰖﰗﰘ
70:39 La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua.
ﰙﰚﰛﰜﰝﰞﰟﰠ
70:40 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza
ﭑﭒﭓﭔﭕﭖﭗﭘﭙ
70:41 Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.
ﭚﭛﭜﭝﭞﭟﭠﭡﭢ
70:42 Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,
ﭣﭤﭥﭦﭧﭨﭩﭪﭫﭬ
70:43 Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo,
ﭭﭮﭯﭰﭱﭲﭳﭴﭵﭶﭷ
70:44 Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa.

Kurani Tukufu


Wednesday, September 9, 2026

Usitusahau katika dua zako njema